
nyumbani salama kwa kusukumwa nje ya gari lililo kwenye mwendo. Eugene Mutuku, mwanafunzi wa KMTC, alifariki mnamo Juni 4, 2026, baada ya kusukumwa nje ya matatu ya Nicco Sacco kwenye Barabara ya Thika. Hili ni tukio la kusikitisha ambalo limeongeza ghadhabu kwa umma kufuatia mfululizo wa visa vya aina hii.
Tukio hili lilitokea mnamo Alhamisi, tarehe 4 Juni 2026. Mwanafunzi huyu wa miaka 19 aliyekuwa akielekea kwenye kliniki yake ya masomo (attachment) Kasarani, alirushwa nje ya basi gogo la matatu na kondakta kufuatia mzozo wa nauli au chenji.
Baada ya kutupwa nje kwenye Barabara ya lami, aligongwa na gari hilo hilo. Kishae alisaidiwa na msamaria mwema na kukimbizwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH), lakini alifariki dunia usiku huo kutokana na majeraha mabaya ya ndani na nje.
Hiki sio kisa Cha kwanza nchini Kenya. Yamekuwepo Matukio Mengine Yanayofanana.na kisa hicho Cha hivi majuzi.Kumekuwa na visa vingine kadhaa vya kinyama ambapo abiria wamejeruhiwa au kupoteza maisha kwa njia hii:
Joseph Mureithi:
Alifariki mnamo Februari 24, 2025, baada ya kusukumwa nje ya matatu ya Super Metro eneo la Kitengela- Namanga kufuatia mzozo.
Gilbert Thuo Kimani:
Alifariki mnamo Machi 2025 kwenye Barabara ya Thika baada ya kutupwa nje ya matatu alipokuwa amebakiwa na shilingi 50 pekee badala ya shilingi 80 za nauli.
Doreen Kinya:
Mwanafunzi aliyeanguka au kusukumwa kutoka kwenye matatu ya Zam Zam Sacco kwenye Barabara ya Thika. Kesi yake ilifikishwa mahakamani na wahusika kufungwa miaka 10 jela.
Hatua za NTSA na Kisheria NTSA: Mamlaka ya Kitaifa ya Usafiri na Usalama (NTSA) imekuwa ikilengwa na lawama kutoka kwa Wakenya wanaodai kwa. kushindwa kuchukua hatua thabiti kudhibiti SACCO zenye utovu wa nidhamu na kutoa mafunzo ya lazima kwa madereva na makondakta.
Hatua za Kimahakama:
Gari la Nicco Sacco lililohusika lilipatikana limeachwa eneo la Kariokor na likapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kasarani. Polisi waliwakamata maafisa wa SACCO, na msako mkali wa kuwasaka dereva na kondakta ambao walizima simu zao na kutoroka unaendelea.
Abiria Wanatakiwa Kufanya Nini?
Ili kukomesha ukatili huu, abiria wanasisitizwa kuchukua hatua zifuatazo wanapokuwa safarini:
Kusaidia inapowezekana:
Iwapo kuna abiria, haswa watoto wa shule, wanaokosa nauli au wanapata shida ya chenji, abiria wengine wanaweza kuchangisha kiasi kidogo na kuwalipia. Hii huondoa mzozo kabisa.
Kupinga Ukatili:
Wasaidie kuzuia utovu wa nidhamu na walazimishe madereva kusimamisha gari ili kuruhusu watu kushuka salama mahali sahihi.Kutoa Taarifa: Piga picha nambari za gari na utoe ushahidi kwa Polisi iwapo tu utashuhudia mzozo unayohatarisha maisha.
Kutoa Taarifa za Ukatili;
Ni vema kwa Wananchi au Raia wote kushirikiana kutoa taarifa kwa Vyombo husika pale Ukatili wa jinsi hii unapofantika.