#OPARANYA''S WOES COULD LEAD TO A U-TURN

 Masaibu makuu yanayomkumba Waziri wa Vyama vya Ushirika na Maendeleo ya Biashara Ndogo Ndogo (MSMEs), Wycliffe Oparanya huenda yakamsukuma

kuhamia Mlengo wa Linda Mwananchi wa Edwin Sifuna. Matatizo hayo yanahusiana na uhaba mkubwa wa fedha katika wizara yake na changamoto za kisiasa katika kuuza sera za serikali ya Kenya Kwanza kwenye ngome inayokabiliwa na  upinzani ni kibarua kizito kwa Waziri huyo.

Pamoja na kwamba hajasema hadharani lakini ukweli unasalia kuwa yumo kwenye Serikali ya Kenya Kwanza kwa kujikokota. Hii inatokana na ukweli Wizara yake imetengwa na kimasilahi na Serikali.

#1. Kwa nini analalamikia serikali ya Ruto kwa kubezwa/kupuuzwa?

Uhaba wa Fedha na Ukosefu wa Utendaji:

 Oparanya amewahi kulalamika waziwazi kuwa ofisi yake inakabiliwa na "vikwazo vikali vya bajeti" kiasi cha kumfanya ajihisi kama "mwombaji". Alieleza kuwa hana pesa za kutosha za kuendesha shughuli za kiofisi na hulazimika kutegemea Makatibu wa Kudumu (PSs) kwa ufadhili wa msingi wakati wa kazi rasmi.

Kazi Ngumu ya Kampeni: 

Oparanya pia amekiri kwamba kazi ya kumfanyia kampeni Rais William Ruto katika ngome za Orange Democratic Movement (ODM) ni ngumu mno. Hii inatokana na hali halisi ya kisiasa kwenye ngazi za chini mashinani na utata wa kuuza sera za serikali ya sasa huku viongozi wa upinzani wakiwa na ushawishi mkubwa. 

#2. Je, atajiondoa kwenye serikali ya Kenya Kwanza?

Hadi sasa, Oparanya hajatangaza kujiondoa rasmi katika serikali ya Kenya Kwanza japo Kuna tetesi kwamba huenda akatathimini ushirikiano wake na Serikali ya Kenya kwanza kwa lengo la kubadili mlengo wa siasa.

Masharti ya Utendaji: 

Ingawa amekuwa akitoa kauli kali kwamba yuko tayari kujiuzulu na kurudi nyumbani ikiwa malengo na mikakati ya maendeleo haitatekelezwa jinsi anavyotaka, bado anaendelea na wadhifa wake japo kama msindikizaji.

Ushirikiano wa Kiserikali: 

Mara nyingi amesisitiza nia yake ya kushirikiana na serikali na kufanya kazi, ingawa anakosoa changamoto zinazomkwaza. 

#3. Upendeleo wa Kiufadhili kwenye Wizara za Serikali:

Malalamiko ya Oparanya ya kukosa ufadhili yanaakisi kile kinachotajwa na wengi kama changamoto ya mgao wa bajeti serikalini ambapo baadhi ya wizara zimependelewa kuliko zingine., lakini kuna mitazamo miwili kuhusu hili:

Ukosefu wa Fedha Kitaifa: 

Serikali yenyewe imekuwa ikilalamikia mapato finyu ya kodi na mikopo iliyopo, jambo linalofanya wizara nyingi kukosa pesa za kutosha za kujiendesha (kama ilivyokiriwa hata na Wizara ya Hazina).

Mvutano wa Kiasiasa:

 Baadhi ya wachambuzi wanaona ugumu wa Oparanya kupata fedha au usikivu wa haraka unatokana na ukweli kwamba yeye na wenzake wanaotoka upande wa upinzani (kama vile wale waliotoka ODM) hawajapewa nguvu kamili au rasilimali zinazolingana na mawaziri wa asili wa muungano wa Kenya Kwanza. 


Post a Comment

Previous Post Next Post