#EBOLA YAUA WATU WATATU KENYA

Ugonjwa wa Ebola ulioripuka mapema mwaka huu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeanza kugharimu maisha ya wakenya hata kabla ya kuripotiwa kisa chochote nchini humo
 Hii ni kutokana na ghasia na maandamano ambayo yameshuhudiwa mara ya pili tarehe 9 Juni 2026 namkuuliwa mtu mmoja kwa kupigwa risasi baada ya makabilano kati ya polisi na waandamani.Hii inafikisha idadi ya watu waliouawa na polisi kwenye maandamano ya Ebola kufikia watatu (3}kwa awamu mbili za  maandamano. Maandamano mengine yalifanyika tarehe 1 Juni 2026 ambapo watu wawili wawili waliofariki kwa kupigwa risasi na polisi.

Hoja ya Msingi:

Ilikuwa ni matarajio ya wananchi wa Laikipia na wakenya kwa jumla kwamba Serikali ingetoa tamko au mwelekeo wa kile kinachopingwa na wananchi kwenye hoja ya Ebola 

Majibu yanayohitajika:

Serikali inatakiwa kuweka wazi au kufafanua hoja ya kuletwa nchini Kenya kwa wamarekani wanaougua ugonjwa wa Ebola au wenye dalili za maambukizi kutoka nchini DRC Congo. Wananchi wa Nanyuki na Kenya kwa ujumla wanaiona  Serikali bado imewaacha gizani bila kujua ukweli kwamba kituo Cha Ebola Cha Laikipia kitakuwepo kwa ajiri ya wakenya pekee au wagonjwa wengine kutoka watapelekwa kwenye kituo hicho. Vituo vya karantini vya Ebola vijengwe kwa ajili ya wakenya pekee si kwa dhumuni la kuleta maambukizi kutoka nje ya Nchi.

Itoshe kusema hapa Kwamba Wananchi wa Nanyuki au wakenya hawapingi kuanzishwa Kwa kituo hicho cha Ebola kwenye Kambi ya Kijeshi ya Laikipia, bali kupelekwa kwenye kituo hicho Wageni Kutoka nje ya Nchi.

Akiongea na maafisa waandamizi wa Wizara ya Afya Harambee House Tarehe 9 Juni 2026, Naibu Rais wa kenya Kithure kindiki amelichukilia kwa wepesi swala hili linalomgharimu maisha ya wakenya kwa kulihusisha na siasa huku akisema akisewa wapo watu miongoni mwa Jamii ambao wamelifanya swala la Ebola kuwa la Kisiasa na kutoa hamasa ya taarifa potofu kwa Umma. Kindiki aliyekwepa kuweka bayana endapo Bado Serikali inao mpango wa kuwahamishia Kenya Wamarekani wanaougua Ebola ambacho ndo kiini Cha ghasia zilizoshuhudiwa Nanyuki.

Haijulikani ni wakenya wangapi watafariki kutokana na kadhia hii ya Ebola kabla ya mwafaka wa swala hili kupatikana. Kinachoonekana kwa sasa ni maandamano na vifo huku Serikali ikisalia kimya kwenye hoja ya wamarekani wanaokusudiwa kuleta maambukizi Kenya 

Hadi kufikia Tarehe 9 Juni 2026, Ebola imegharimu maisha ya watu watatu katika mji wa Nanyuki kutokana na maandamano ya Kupinga kuanzishwa Kwa kituo Cha karantini kwa ajili ya wamarekani wenye Ebola wanaokusidiwa kuhamishiwa kwenye kituo kinachojengwa kwenye Kambi ya Kijeshi ya Laikipia.

MATUKIO YA NYUMA

Jumatatu, Juni 1, 2026, maeneo ya Nanyuki (Kaunti ya Laikipia) na baadaye wanaharakati wakaandamana jijini Nairobi.

Dondoo na Hoja:

 Mamia ya wananchi na wanaharakati waliingia mitaani wakipinga vikali mpango wa kuanzisha karantini ya wagonjwa wa Ebola katika Kambi ya Jeshi la Anga ya Laikipia. Walitaka kujua usalama wa jamii zinazozunguka kambi hiyo endapo virusi vitaenea, wakidai hawakushirikishwa katika uamuzi huo wa siri. 

Maandamano hayo yalisababisha ghasia zilizoripotiwa kuua watu wawili. Ubalozi wa Marekani ulitoa tahadhari ya usalama kwa raia wake.

Kumb:

Tarehe 3 Juni 2026 mtandao huu uliripoti kuwepo wingu la maandamano kujirudia tena kwa wakazi wa Nanyuki au hata kote nchini Kenya.

Post a Comment

Previous Post Next Post