#MAJAMBAZI WALIOMVAMIA SENETA WA VIHIGA NI VIGOGO WENYE PESA

 Tar 17 aprili 2026, Mahakama ya mjini kisumu imetoa ridhaa ya kuachiwa kwa dhamana watuhumiwa watatu (3) wa kosa la kumvamia kumpiga na kumjeruhi vibaya Seneta wa Vigiga Godfrey Osotsi mjini Kisumu Tar 8 Aprili 2026, Baada ya mahakama kujiridhisha kwamba upande wa mashataka haukutoa sababu za msingi kuishawishi kuwanyima watatu hao dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena Tarehe 6 Aprili 2026

Watuhumiwa hao wamepewa dhamana inayowahitaji kulipa kiasi Cha pesa za Kenya Sh.Milioni moja kila mmoja na kuwa na mdhaminj ambaye pia ataweka kiasi sawa na hicho.

Lakini kinachoshangaza kwetu sisi si hoja walah haki ya kupewa dhamana ila kiasi Cha fedha ya dhamana kwa watuhumiwa na wadhamini wao. Mara nyingi pamekuwepo misemo na kauli zinazosemwa kwamba watu/vijana wanaotumiwa kwenye visa vya kihuni na ujambazi kwenye milengo ya kisiasa ni vijana ambao aidha hawana ajira Wala kazi, na hurubuniwa kwa kupewa fedha kidogo mathalani hata sh. 1.000/- ili kufanya uhalifu.

Sasa inapofikia kwamba mtu aliyenunuliwa kwa kupewa pesa ndogo kama hiyo anaweza kupata pesa kiasi Cha Sh Milioni moja kulipia dhamana ni jambo la ajabu. Hii maana yake ni kwamba hao mnaowaona si Wahusika. Wahusika ni Vigogo wa Kisiasa au wa Serikali.

Tuchukulie mfano wa maandamo ya vijana wa kizazi kipya, Gen Z. Vijana wengi waliokamatwa katika Matukio yale hawakuweza kulipa dhamana hata ya Sh50,000/- na tulishuhudia baadhi ya wazazi wakilalamikia dhamana kubwa kwa watoto wao.

Leo hii tumaona kwamba vijana hawa kwenye kesi hii inayoendelea kwenye mahama mjini kisumu wakiwa na uwezo wa kulipa fedha za ukwasi kama dhamana.

Sasa kwa vile serikali imekiri kukamatwa kwa watuhumiwa wengine wa uhalifu unaoshabihiana na huo mjini Kitale na Nairobi, tunayo hamaki ya kuona mwenendo wa mashataka yao na hali halisi ya dhamana zitakazotolewa katika kesi hizo.


Post a Comment

Previous Post Next Post