#BITOK ALIPASWA KUFUTWA KAZI NA SI KUHAMISHWA

Taarifa za hivi punde zinazohusiana na kuhamishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara

ya Elimu, Idara ya Elimu ya Msingi kutoka Wizara hiyo kwenda Wizara ya Utalii inasikitisha. Kwa mujibu wa taarifa fupi iliyopeperushwa na kituo Cha Runinga ya Citizen, Julius Bitok amehamishiwa kutoka Wizara ya Elimu kwenda Wizara ya Utalii kwa kumbadilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii John Lekakeny Oloituaa kuchukua nafasi yake.

 Makatibu wote wawili waliobadilishana nafasi hizi ni miongoni mwa Makatibu Wakuu wengine lukuki kwenye Wizara zingine wanaotoka eneo moja la bonde la ufa na Rais Ruto katika uteuzi wake alioufanya kipindi ameingia madarakani.

Tunadhani ni vema ifike sehemu Serikali ya Rais William Ruto ionyeshe uwajibikaji. Endapo Waziri huyu ameyakoroga kwenye Wizara ya Elimu kwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa sera na Mipango madhubuti ya wizara ya Elimu, kwanini ahamishiwe kwenye Wizara nyingine? Hatua hiyo ni kutoa mwanya ili ili pia akaharibu huko?

Aliyekuwa Katibu wa Wizara ya Utalii nchini Kenya John Lekakeny Ololtuaa ambaye Katika mabadiliko ya hivi punde amehamishiwa kutoka Wizara ua Utalii hadi Wizara ya Elimu ni msomi mwenye shahada ya Uzamili.

Shahada ya Kwanza:

 Ana Shahada ya Elimu (Sanaa) kutoka Kenyatta University.

Shahada ya Uzamili: 

Ana Shahada ya Uzamili (Master's) katika Usimamizi wa Elimu (Education Administration) kutoka chuo kikuu hichohicho cha Kenyatta 

University.Uzoefu: 

Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu, alikuwa mtaalamu wa elimu aliyefanya kazi kama mwalimu, mkuu wa shule, Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti (kwa Kaunti za Bomet na Kajiado), na Mkurugenzi wa Elimu wa Kanda nchini Kenya.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu (au Katibu wa Idara ya Elimu ya Msingi), Prof. Julius Bitok, ana kiwango cha Shahada ya Uzamifu (PhD) katika Usimamizi wa Biashara kutoka Oklahoma State University nchini Marekani.

Viwango vyake vya kitaaluma vinajumuisha:

Shahada ya Uzamivu (PhD): 

Usimamizi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Oklahoma State University.

Shahada ya Uzamili (MBA): Utawala wa Biashara (Business Administration).Shahada ya Kwanza: Uchumi.



Post a Comment

Previous Post Next Post