Chama chama Orange Democratic Movement (ODM) Cha kenya hasa mlengo wa Linda Ground, kimedokeza uwezekano wa kutosimamisha mgombea
wa Urais mwaka ujao wa 2027 ili kumpa kukusanya Nguvu kumpa ushindi Rais Ruto. Katika mkakati wake, Cha hicho kimepania kutumia idadi kubwa ya wabunge wake kujenga ushawishi na nguvu za kisiasa zitakazokiwezesha kuingia kwenye serikali ijayo kupitia muungano wake na chama cha UDA. Haya hivyo chama hiki Cha ODM kinakabiliwa na mambo makuu yafuatayo:1. Kughairi Kusimamisja Mgombea Urais:
Uamuzi huu unatokana na mkakati wa chama cha ODM wa kutaka kushiriki moja kwa moja katika serikali kuu. Badala ya kupoteza nguvu na rasilimali nyingi kupambana na muungano unaotawala, chama kinalenga kutumia wingi wa viongozi na wawakilishi wake kushirikiana na vyama vingine ili kiwe na hisa (shares) kubwa katika serikali itakayoundwa.
2. Uamuzi wa Kutoshiriki:
Hoja ya kutokuwa na mgombea urais imebainika lini? Uamuzi huu na mwelekeo mpya ulianza kujulikana wazi mwezi Mei 2026 wakati Kiongozi wa chama hicho, Dkt. Oburu Oginga, alipoweka wazi nia yake ya kutetea kiti chake cha Useneta badala ya kuwania urais kama wengi walivyodhania.
Hii ilifuta kabisa dhana ya chama kusimamisha mgombea binafsi ngazi ya urais na badala yake kuelekeza nguvu kwenye ngazi za chini. Lakini hapa Kuna hoja nyingine inazuka hapa kwamba ilikuwa ni lazima Oburu Oginga agombee ndipo chama kisimamishe mgombea? Hapo Kuna karata imechezwa maana hiyo haiwezi kuwa sababu.
3. Mgawanyiko wa Milengo Miwili:
Kuna mgawanyiko wa wazi kati ya mlengo wa "Linda Ground/Mwananchi" unaounga mkono mazungumzo ya karibu ya kisiasa na serikali ya Rais William Ruto, na mlengo wa upinzani ndani ya chama ambao unapinga mazungumzo hayo ya haraka. Hali hii inatishia mshikamano wa chama na kuathiri maamuzi ya mwisho.
4. Hatima ya Ushiriki wa ODM kwenye Serikali Ijayo:
Kufanikiwa kwa azima ya ODM kutategemea uwezo wao wa kuweka nyumba yao sawa na kusimama kidete kwenye meza ya mazungumzo na vyama washirika. Hata hivyo, kutokana na misingi na taratibu zilizopo za kisiasa, kufanikiwa au kutofanikiwa kwake kumejaa utata kutokana na makundi kinzani.
5. Hatari ya viongozi wa ODM kupoteza viti vyao:(Arati, Wanga, Junet, Oburu)
viongozi hawa mashuhuri wanampigia upatu ushirikiano wa chama hicho na Serikali ya UDA huenda wao wenyewe wakakabiliwa na upinzani mkali majimboni kwao. Hali hii inatokana na hatari ya kupoteza uungwaji mkono kutoka kwa wananchi wanaokerwa na msimamo wa viongozi hao wa kushirikiana na serikali, hali inayoweza kuwapunguzia mvuto na kuwapa wakati mgumu katika utetezi wa nafasi zao.
6. Mivutano wa Ugavi wa asilimia 50 kwa 50 kati ya ODM na UDA: Madai ya ODM kutaka mgawo wa 50% ya uongozi serikalini yanasababisha mivutano kati ya muungano unaotarajiwa.
Chama cha UDA chenyewe hakina budi kuwagawa vyeo na kuungana na vyama vingine vya kisiasa, jambo linalofanya kuwa vigumu kukubali kutoa nusu nzima ya serikali kwa chama cha ODM pekee bila kushirikisha vyama vingine vinavyounga muungano huo.
7. Shinikizo la ODM kutaka nafasi ya Naibu Rais:
Chama Cha ODM kinasisitiza kwamba iwapo chama kitakachoshika urais (kama UDA) kinatoka upande mmoja, basi nafasi ya Naibu Rais lazima iende upande wa ODM ili kupata uwiano. Hata hivyo, hili ni suala gumu na tata kwani nafasi hiyo kwa sasa inashikiliwa na wanasiasa kutoka eneo la Mlima Kenya ambao hawatakuwa tayari kuachia nafasi hiyo kwa urahisi.
Haya ndo baadhi ya mambo yatakayosababisha miungano au ubia wa madaraka ya kuongoza Serikali ijayo kusambaratika kwa vile hayatawezekana.
Toa maoni yako....
