#What Causes Dry Spell?


 #"Dry Spell" ni hali linalowakumba wanawake japo viwango vyake huachana kutoka kwa mmoja hadi mwingine.

"Dry spell" ni kipindi ambacho mwanamke haonekani kuwa na hamu ya tendo la ndoa, haoni mwamko au hamu ya mwili, au hapati fursa ya kushiriki tendo la ndoa kwa muda fulani (wiki, miezi, au miaka). 

#1. Nini husababisha "Dry Spell"?

Mabadiliko ya Hormoni: Kupungua kwa "estrogen" wakati wa kukoma hedhi (menopause), kunyonyesha, au kutumia vidonge vya uzazi wa mpango.

Msongo wa Mawazo (Stress): 

Kazi nyingi, shida za kifedha, au wasiwasi. Matatizo ya Uhusiano: Ugomvi, ukosefu wa mawasiliano, au kutokuelewana na mwenzi.

Uchovu:

 Uchovu wa mwili au akili unaweza kusababishwa na mrundokano wa mambo mengi.

Umri:

Wanawake wenye umri mkubwa wanaweza kukabiliwa na tatizo hili kutokana na maumbile.

2. Mwanamke anayepitia hali hii afanye nini?

Kutumia vilainishi (Lubricants): Kununua vilainishi vya maji ili kupunguza maumivu na ukavu wakati wa tendo.

Kuzungumza na Mwenzi:

 Ni vema kuongea na kujadili shida zenu waziwazi bila ifichonau kulaumiana.

Kupunguza Msongo:

 Kupumzika, kufanya mazoezi, na kupunguza kazi.

Kuona Daktari:

 Kumuona daktari wa magonjwa ya wanawake (Gynecologist) ili kupima hormoni. 

3. Je, kupata mpenzi ni tiba?

Si lazima ila mara nyingi hutegemeana na chanzo. Kupata mpenzi hakumalizi shida ikiwa chanzo ni msongo wa mawazo au kutokuelewana. Tafiti zinaonyesha kuwa hata walioolewa wanaweza kupitia ukame wa tendo la ndoa. 

4. Je, mwanamke anaweza kupitia 'dry spell' akiwa na mume/mwanamume?

Ndiyo. Mwanamke anaweza kuwa na mume na bado akapitia 'dry spell' kama hana hamu ya tendo au anafanya tendo kwa kulazimika (painful intercourse). Hii hutokea wakati hisia na muamko wa mwili unapopungua, hata kama tendo lenyewe linaendelea kufanyika.

Post a Comment

Previous Post Next Post