#NINI Kifanyike kumaliza Dhuluma za Kijinsia kuwa Janga la Kitaifa ni Suluhu?

 Hivi karibuni imetolewa miito kwa Serikali kutangaza kwa visa vya Ukatili au Dhuluma za kijinsia kuwa

Janga la kitaifa. Hoja yetu hapa ni kwamba je hiyo inaweza kuwa Suluhu? Kwa maoni yetu tunadhani ipo haja ya kufanyika jitihada za makusudi kukabiliana na tatizo hili mbali na kutangazwa kuwa Janga la kitaifa. Hatukatai wito huo isipokuwa hatua hiyo Bado si Suluhu.

Katika kutekeleza azima hiyo ni lazma chanzo au kiini Cha tatizo kijulikane na hatua madhubuti kuchukuliwa. Tofauti na hivo inawezekana kutangazwa hivo na bado tatizo likaendelea. Hapa Kuna mapendekezo yetu:

i)  Utekelezaji thabiti wa sheria: Kutoa adhabu kali na za haraka kwa wahalifu ili kuondoa utamaduni wa kutoadhibiwa na kuhakikisha vyombo vya usalama vinachukua hatua za dharura mara tu visa vinaporipotiwa.

ii? Uhamasishaji na elimu: Kuelimisha jamii, hususan wavulana na wanaume, ili kubadili mtazamo na mfumo dume unaochochea chuki na unyanyasaji dhidi ya wanawake.

iii? Vituo vya usaidizi: Kuongeza vituo vya kutoa hifadhi salama (safe houses) na huduma za msaada wa kisaikolojia kwa waathiriwa walio katika hatari.

iv) Uwezeshaji wa kiuchumi: Kuwapa wanawake uhuru wa kifedha ili kuepuka utegemezi unaowafanya wanase katika ndoa au mahusiano yenye ukatili.

v) Kuripoti visa: Jamii inapaswa kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa za siri kupitia namba za dharura za polisi (kama vile 112 au 999) au kupitia mashirika kama vile UNHCR Kenya.

vi) Elimu na ushauri kwa wanawake na watoto wa kike Kuhusu mahusiano na kuwa wepesi wa kugundua Wanaume wenye Nia mbaya, kuwa wepesi kujiondoa kwenye mahusiano yaliyochacha.

vii) Utoaji wa Elimu na Uhamasishaji kwa vijana kuepuka matumizi ya mihadarati vinavyosababisha kufikiwa maamuzi magumu.

viii) Uwezeshaji wa nafasi za ajira kwa vijana na ushauri nasaha kupunguza msongo wa mawazo kwa vijana.

Kulingana na mashirika ya kutetea haki za wanawake nchini Kenya, hakuna idadi kamili ya kitaifa iliyotolewa na serikali, lakini ripoti zinaonyesha kuwa zaidi ya wanawake 27 waliuawa kikatili katika kipindi cha kwanza cha mwaka huu kufikia mwezi Mei. Hata hivyo, makadirio ya Umoja wa Mataifa huweka wastani wa vifo 47 vya wanawake kila wiki nchini Kenya. 

Baadhi ya visa vichache tulivyoweza kupekua kwa kipindi Cha Januari hadi Mei 2026 ni pamoja na:

Kisa kilichofungua mwaka 2026 ni Cha Ukatili wa mzazi kwa mtoto kililipotiwa eneo la Dandora, Nairobi,Januari Mosi 2026, Cha mtoto Charlene Nyangweso aliyeadhibiwa kwa kupigwa vibaya na baba yake na kumsababishia kifo, baba yake aliyekuwa ametengana na mama ya mtoto alimwadhibu kwa kosa la kwenda kutembelea mama yake na kuchelewa kurudi.

Visa vinginevyo tulivyoweza kubainishwa taarifa zake ni pamoja na :

#1. Davine Kwamboka (Kaunti ya Migori): Aliuawa kikatili mwezi Aprili, ambapo picha za CCTV zilionyesha mumewe na wanaume wengine wakijaribu kutupa mwili wake.

2. Anita Nyambura (Kaunti ya Nakuru): Aliuawa mwezi Aprili na mumewe ambaye ni mwanajeshi (KDF) mbele ya mtoto wao mchanga.

3. Benedicta Keziah (Kaunti ya Kilifi): Msichana wa umri wa miaka 7 ambaye aliuawa kikatili mnamo mwezi Mei, tukio lililozua hasira kali nchini.

4. Shirley Gatumi (Kaunti ya Tharaka Nithi): Msichana wa miaka mitatu aliyetoweka mnamo Mei na mwili wake kupatikana ukiwa umetenganishwa viungo.

5. Winny: Mwanamke mwenye umri wa miaka 23 aliyepatikana amefariki katika Kijiji cha Kamuga, Nyakach, mnamo Mei 12 baada ya kushambuliwa na mumewe katika mzozo wa nyumbani.

6. Rose Apundi (au Rose Benta Aponia): Mwanafunzi wa miaka 21 wa Riat College ambaye alitoweka Aprili 5, na mwili wake wenye majeraha kupatikana siku chache baadaye ukiwa umetupwa kwenye msitu wa Riat, eneo la Kisumu.

7. Roseline Achieng Odhiambo: Mwanamke wa miaka 37 aliyepatikana Nyumbani mwake, akiwa amefariki na akiwa na majeraha mengi mwilini mwake katika mtaa wa Manyatta 'B' kufuatia shambulio linalohusishwa na unyanyasaji wa nyumbani. 

#8.  Ann Keya Ahuna aliyeuawa 16 Mei 2026 kwa kuchomwa Kisu na mtu anayesadikiwa kuwa mpenzi wake kwa jina Newton Ambeyi.

9. Sheila -- Kutoka Nyamira Ekerenyo Mwanafunzi mwenye umri miaka 16 aliyeuawa na mtu anayesadikiwa kuwa mpenzi wake ambaye alijinyonga baada kutekeleza kisa hicho.

10. Rachel Wandetto: Mwanamuziki aliyefariki mnamo Mei 19, 2026 baada ya kushambuliwa na kuchomwa moto na watu wasiojulikana.

11. Mercy Nyambura -- Mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Sinendet aliyetoweka Mei 18-19,2026 baada ya kutoweka na kupatikana akiwa amekufa kwenye shamba la mahindi.

12.) Abigael Nafula Ogara (32) aliyetoweka Aprili 29,2026 na mwili wake kupatikana kwenye chumba na maiti webuyeMei 22,2026. Inahisiwa kuwa Mwenzi wake askari KDF Bonface Somiyu huenda alihusika na kutoweka kwake, alionekanannaya mara ya mwisho.

13.) Alice Riang'a kutoka Itibo, Suneka Kisii alitoweka Mei 6, 2026, baadaye mwili wake ulipatikana msitu wa Barkowino, Bondo.alizikwa Mei 22, 2026.

14.) Mwanamke kwa jina Jackline Wanjiru (27) alishambuliwa na kumwagiwa Tindikali kwa kile kinachoaminika kama Dhuluma ya kimapenzi, eneo la Kiritili, Embu hatimaye alifariki dunia, Alizikwa Mei 27,2026.

15.) Mwezi wa nne 2026,Mwanamke kwa jina Mercy Awour aliviziwa na kumwagiwa Tindikali na mtu anayesadikiwa kuwa mpenzi wake aliyetumia pikipiki usafiri  na kutoweka baada ya tukio hilo.

16. Tarehe 18 Mei, 2026, Mwanamke kwa jina Maurine Masili anauguza majeraha baada ya kudaiwa kumwagiwa maji ya maharage yaliyokuwa yakipikwa jikono baada ya mzozo kuibuka kuhusiana na ubishi juu ya ongezeko la Bei ya Mafuta na msimamo wake kauli ya ''tutam:

17. Mwezi Mei 26, 2026 Mwanafunzi wa kidato Cha nne (17) huko Nakuru anadaiwa kumwagiwa Tindikali na mwanaume 22) anayedaiwa kumlazimisha awe mchumba wake na baada ya kukataliwa alimvizia binti huyo mapema asubuhi akienda Shule na kumwagiwa Tindikali.

18. Mwezi Mei 27, 2026 eneo la Shieni Kaunti ya kirinyaga Mwanaume wa miaka (45) anadaiwa kumuua mpenzi wake mpenzi wake umri miaka (39) baada ya kuibuka mzozo Naina Yao.

19. Tarehe 14Juni, 2026, Mwili wa mwanamke kwa jina Mwanahamisi Juma ulipatikana ukiwa umetupwa kichakani Kijiji Cha Ziwani, eneo la Matuga, kwale kwa kile kinachoaminika alifanyiwa Ukatili kabla ya kuuawa. Mwanamke huyo alikuwa ni bubu.

20. Tarehe 11, Juni 2026, Mwili wa Mwanamke kwa Jina Joy Kwanini Gathu ulipatikana kwenye gunia ukiwa umekatwakatwa vipande na kutupwa huko Nyeri. Mwanamke huyo alikuwa na umri wa miaka 25, Muhitimu wa chuo Cha Nyeri Polytechnic.

21. Tarehe 02 Juni 2026, mwili wa Mwanamke kwa Jina la Salome Chelagat ulipatikana ukiwa uchi kitandani mwake kwenye nyumba ya kupanga eneo la Mucherwo, Molo Kaunti ya Nakuru.

22..Tarehe 19, Juni 2026, Mwili wa mwanamke kwa jina la Susan Wanjiku Njeri ulitambuliwa na ndugu zake njia alama za vidole na Msimbogeni baada kutoweka kati ya tarehe 11-12, Juni 2026 kutoka eneo la Cieko Kasarani alipokuwa ameanza kazi za ndani (Yaya).

Hivi ni baadhi ya visa vichache tu lakini uhalisia ni zaidi ya idadi hii.

Toa maoni Yako.....



Post a Comment

Previous Post Next Post