Mpekuzi halisi imebaini mara kadhaa matumizi ya lugha ya kiingereza zaidi ya kiswahili kwenye Kipindi Cha
'Uliza Dakitari' kinachorushwa na Runinga ya Citizen kila Jumapili saa 2.00 usiku.Dakitari Lauryn Mengesa ambaye ni mwandaaji Mtangazaji na Mtangazaji wa kipindi hicho hutumia lugha ya kiingereza zaidi na Wageni wake kuliko kiswahili. Kwa maoni yetu hali hii inapoteza mantiki ya lengo la kipindi hicho kuwa Cha kiswahili. Katika dodoso letu tulibaini sababu zifuatazo zinazopelekea matumizi ya lugha ya kiingereza kuliko kiswahili:
Istilahi za Kitabibu:
Dkt. Lauryn Dkt. Lauryn B. Mengesa ni daktari bingwa wa uzazi na magonjwa ya wanawake Dkt. Lauryn B. Mengesa. Mara nyingi hutumia maneno ya Kiingereza kwa sababu istilahi nyingi za kisayansi na matibabu hazina tafsiri rahisi au inayoeleweka kwa urahisi katika Kiswahili sanifu.
Lugha ya Majadiliano:
Hata pale anapoelezea magonjwa, hutokea akachanganya lugha hizo mbili ili kurahisisha kueleweka kwa watazamaji wasio na taaluma ya afya, ingawa wakati mwingine uwiano unakuwa mkubwa zaidi upande wa Kiingereza.
Tumehoji haja ya Mkalimani au tafsiri ya maelezo yanayotolewa kama inavyostahili kwa Vyombo vya habari komavu na kubaini:
Jukumu la Mtangazaji:
Uhitaji wa mkalimani hutegemea mtayarishaji wa kipindi (Citizen TV). Kwa kawaida wageni wanaoitwa huwa na uwezo wa kueleza masuala hayo, lakini kuna wakati watazamaji huhoji iwapo lugha iliyotumika ilikuwa ngumu sana kueleweka bila tafsiri.
Tatizo Sugu la Vyombo vya habari
Aidha tatizo hili halijitokezi kwenye Runinga ya Citizen pekee ila karibu kwenye Vyombo vyote vya habari vya Kenya. Utakuta mgeni anaalikwa kwenye mahojiano ya kiswahili kwenye Redio au Runinga na anaishia kuongea kiingereza kipindi kizima, mbaya zaidi hakuna tafsiri yoyote inayofanyika.
Hili ni suala linaloonekana mara kwa mara katika vyombo vya habari vya Kenya. Vipindi vingi vinavyojadili mambo ya kitaalamu (sheria, afya, uchumi, au teknolojia) huwa na changamoto ya kusawazisha kati ya lugha rasmi ya kipindi na istilahi ngumu za kitaalamu zinazopatikana zaidi katika lugha ya Kiingereza, jambo linaloleta mjadala mkali kuhusu uhalisia na ukiukaji wa msingi wa lugha ya Kiswahili.
Hata hivo si Kwamba hakuna maneno ya kiswahili yanayoweza kutumika, ila ni changamoto za udhaifu wa watangazaji na wandaaji wa vipindi vya Redio na Runinga.
Kuhusu utata wa matumizi ya lugha hizo, yafuatayo ndiyo maelezo ya kina:
Lugha ya Kipindi:
Lugha kuu ya kipindi ni Kiswahili na inasemekana lengo ni kurahisisha ufahamu kwa wananchi wengi wa kawaida. Hata hivyo, mara nyingi mada za kitiba huhitaji istilahi ngumu (medical terms) ambazo ni rahisi zaidi kuzieleza au kueleweka kwa Kiingereza. Lakini huyo Mwananchi wa kawaida atafikiwa vipi endapo lengo la kipindi linabatilishwa?
Matumizi ya Kiingereza:
Dkt. Lauryn Mengesa hutumia Kiingereza zaidi au kuchanganya na Kiswahili kidogo ili kuhakikisha kuwa maelezo ya kitaalamu yanabaki sahihi (accurate) na kuzuia upotoshaji wa taarifa za kiafya unaoweza kujitokeza wakati wa kutafsiri istilahi za afya moja kwa moja.
Hadhira Inayolengwa:
Licha ya kuwa lengo ni kuwafikia wengi, kipindi hiki hutoa nafasi pia kwa madaktari na wataalamu bingwa kueleza chanzo cha magonjwa, kinga, na matibabu kwa njia ambayo mtu wa kawaida anaweza kuielewa kupitia lugha zote mbili mchanganyiko (code-switching).
Hoja ya Msingi:
Hoja yetu hapa ni kwamba hakuna neno lolote la Kitaalamu linalotumika kwenye lugha ya kiingereza katika enzi hii ambalo halina tafsiri ya kiswahili. Na je, wakenya wote wanajua kiingereza? Kama.sivyo basi kiswahili kinasalia lugha mwafaka ya Kitaifa.
Kama lengo na dhima ya kipindi ni kutangaza kwa kiswahili, Kwanini lugha ya kiswahili isizingatiwe?
Na je endapo haja ya matumizi ya kiswahili ni kuifikia hadhira kubwa, lengo hili litafikiwa vipi endapo kipindi Cha kiswahili kitageuzwa kuwa cha kiswahili mwanzo mwisho?
Kwa mantiki hiyo maana ya kipindi hicho kuwa Cha kiswahili inapoteza ambapo ni Bora kisalie kuwa cha kizungu.
Wageni au Wataalamu Wanaoalikwa:
Ni jukumu la Mtangazaji au mwandaaji wa kipindi kujua endapo mgeni wake hajui kiswahili ili aandae mazingira ya kutafsiri kile kinachojadiliwa.
Katika falsafa na Taaluma ya Uandishi wa Habari na Utangazaji, habari ni mithili ya chakula kinachoandaliwa kwa mlaji. Sasa pale unapoandaa chakula bila kujali nani wa kukila ni tatizo. Moja ya misingi mikubwa ya habari ni lugha ya mlaji ambayo ni ile hadhira yenyewe.
Kitika Kipindi ChaUliza 'Dakitari' Cha Jumapili ya Tarehe 17 Mei 2026, Dr Lauryn Mengesa alikuwa na Mgeni studio kwa Jina la Dr Mohamed Jeilan. Katika mahojiano yaliyofanyika, Dr Jeilan alitumia lugha kiingereza mwanzo hadi mwisho wa kipindi na hakuna tafsiri iliyofanywa na mwongozaji wa Kipindi ambaye pia alifuata mkondo sawia.
Kuna baadhi ya watazamaji waliopiga simu studio kuuliza maswali kwa kiswahili lakini maelezo yalitolewa kwa kizungu. Japo ndipo tunapohoji kwamba je endapo aliyepiga simu hajui kiingereza,je ujumbe ule ulimfikia mlengwa? Vipi kuhusu watazamaji wengine ambao hawana fursa ya kuhoji?
Katika mazingira kama haya je Kuna haja ya Kipindi hicho kuwa cha kiswahili?
HITIMISHO:
Watangazaji na wandaaji wa vipindi ni vema wazingatie lugha zilizowekwa kwenye lengo, dhima na dira na maudhui ya vipindi husika.
Toa maoni yako....
