JE, UNAFAHAMU SABABU ZA 'DRY SPELL?'

  Kipindi ambacho mwanamke huwa na hali ya Ukavu/ ukame

kwenye uke wake au kwa kiingereza (dry spell/husababishwa na mambo mengi.

Tafsiri halisi ya "Dry spell" ni kipindi ambacho mwanamke haonekani kuwa na hamu ya tendo la ndoa, haoni muamko wa mwili, au hapati fursa ya kushiriki tendo la ndoa kwa muda fulani (wiki, miezi, au miaka). 

1. Nini husababisha "Dry Spell"?

1. Mabadiliko ya Hormoni: Kupungua kwa "estrogen" wakati wa kukoma kwa hedhi (menopause), kunyonyesha, au kutumia vidonge vya uzazi wa mpango.

2. Msongo wa Mawazo (Stress): Kazi nyingi, shida za kifedha, au wasiwasi.

3. Matatizo ya Uhusiano: Ugomvi, ukosefu wa mawasiliano na mwenzi, au kutokuelewana na mwenzi.

4. Uchovu: Uchovu wa mwili au akili. 

HATUA ZA KUCHUKUA

 Mwanamke anayepitia hali hii afanye nini?

1. Kutumia vilainishi (Lubricants): Kununua vilainishi vya maji vya kipakaankwenye uke ili kupunguza maumivu na ukavu wakati wa tendo.

2. Kuzungumza na Mwenzi: Kujadili shida zenu waziwazi bila kulaumiana.

3. Kupunguza Msongo: Kupumzika, kufanya mazoezi, na kupunguza kazi.

4. Kuona Daktari: Kumuona daktari wa magonjwa ya wanawake (Gynecologist) ili kupima kiwango cha hormoni. 

3. Je, kupata mpenzi ni tiba?

Hilo Si lazima. Kupata mpenzi hakumalizi shida ikiwa chanzo ni msongo wa mawazo au kutokuelewana. Tafiti zinaonyesha kuwa hata walioolewa au wanawake wenye wenzi wao wanaweza kupitia ukame wa tendo la ndoa. 

4. Je, mwanamke anaweza kupitia 'dry spell' akiwa na mume/mwanamume?

 Mwanamke anaweza kuwa na mume na bado akapitia 'dry spell' kama hana hamu ya tendo au anafanya tendo kwa kulazimika (painful intercourse). Hii hutokea wakati hisia na muamko wa mwili unapopungua, hata kama tendo lenyewe linaendelea kufanyika.

Je, wewe ni mmoja wa wanawake wanaopitia katika jali kama hii? Tupatie maoni yako kwa ushauri nasaha.

Post a Comment

Previous Post Next Post