MOST POPULAR

#JE, UDHANI KUNA HAJA YA MAANDANO KUSHINIKIZA PUNGUZO LA BEI YA MAFUTA?

Tunakuuliza kwenye jukwaa hili, Je, unadhani Kuna haja ya kuwepo maandamano nchini Kenya Kushinikiza punguzo la bei ya mafuta?

 Tumewaona viongozi wa mlengo pinzani wakitoa hamasisho kwa Umma kwenye majukwaa na mtandaoni  kuhusu maandamano ambayo awali yalipangwa kufanyika Jumanne, Aprili 21, 2026, nchi mzima chini ya hashtag #RejectFuelPrices na #RejectSelfishness. Kiongozi wa Third Way Alliance, Ekuru Aukot alinukuliwa akisema waziwazi kuwa atashiriki na kuunga mkono maandamano hayo kupinga bei ya juu ya mafuta.

Miongoni mwa Viongozi wa Upinzani wanampigia debe kifanyika maandamano hayo ni kinara wa DCP Rigathi Gachagua pamoja wenzake wa mlengo huo.

Katika taarifa zilizopatikana leo Tar 18 Aprili 2026, kupitia citizen tv, Rigathi Gachagua ametoa shinikizo la sikunsaba serikali iwe imepunguza bei ya mafuta.

Je, yatafanyika?

Ingawa uhamasishaji ni mkubwa, Kamanda wa Polisi wa Nairobi, Issa Mohamud, alishatangaza maandamano hayo kuwa haramu, akisema waandalizi hawakutoa taarifa rasmi kwa polisi. Licha ya hayo, maandamano mara nyingi huendelea bila ruhusa ya polisi. Sisi tunadhani kabla ya mwananchi wa kawaida kutoka kwenda kuandamana Kuna haja ya kuangalia mambo ya msingi.

Hatua ya Serikali (Kupunguza VAT na Bei ya Mafuta)

1. Tarehe 16 Aprili, 2026, Rais William Ruto alitia saini Mswada wa Marekebisho ya VAT, ambao ulipunguza VAT kwenye mafuta kutoka 16% hadi 8% kwa miezi mitatu. Hii ilisababisha kushuka kwa bei ya petroli (kwa takriban KSh9) na dizeli (kwa takriban KSh10). Hata hivyo, waandamanaji wanahisi hii haitoshi kupunguza gharama kubwa ya maisha.

2. Kama hatua ya dharula, Bunge la kitaifa liliridhia na kuupitisha mswada wa marekebisho ya kupunguza Kodi ya ongezeko la thamani, yaani VAT ili kumlinda mtumiaji wa chini hatua iliyowezesha kwa bei tajwa hapo juu.

3.Wanasiasa wa upinzani hawajatoa hoja makini zenye uzito kushawishinUmma kwamba Rais Ruto anayo maslahi katika kupanda kwa bei ya mafuta.

4. Swala la.kupanda kwa bei ya Mafuta hakujaiathiri Kenya pekee, bali ni swala mtambuka, Dunia mzima inalia.

5. Viongozi wa Upinzani wanatumia mtaji wa kuongezeka kwa bei ya mafuta kujiimarisha Kisiasa.

6. Serikali inapaswa kupewa muda kutafakari manunuzi au uagizaji wa Mafuta kwa mikataba ya (G-G) kwa maana ya kuuziana serikali kwa Serikali kama isipokuwa tija ili ubadilishwe.

7. Kuna taarifa kwamba Serikali ya Kenya imeomba fedha au msaada wa dharula kutoka Benki ya Dunia ili kukidhi ongezeko la bei ya mafuta.

8. Rigathi Gachagua ambaye hivi leo yuko mstari wa mbele kushawishi Umma kuandamana alikuwepo kwenye Serikali ya Rais Ruto na alishiriki kuingia mikataba wa G-G ambao leo anaupinga.

9. Serikali inapaswa kusimamia vyama au Miungano ya wasafirishaji hasa ni lazika wafuate maelekezo ya serikali, bei ya mafuta inaposhuka na wao washushe nauliza. Inasikitisha kuona eti kiongozi au Mwenyekiti waa kukataa kwamba hawawezi kushusha nauliza baada ya kupandisha. Kwa Tabia hiyo juhudi za serikali hazitakuwa na maana kwa Wananchi wa kawaida.

Athari za Maandamano

Kisisasa/Kijamii: 

Mvutano wa juu wa umma na shinikizo kwa utawala wa Rais Ruto.

Kiuchumi: 

Uwezekano wa kufungwa kwa biashara jijini Nairobi na miji mikubwa.

Usafirishaji:

 Usumbufu wa sekta ya uchukuzi na uzalishaji.

Usalama: 

Hatari kubwa ya mzozo kati ya polisi na waandamanaji, kwani mwaka 2026 umewekwa alama ya kuwa na mivutano mikubwa ya kisiasa.

Uelewa wa Mgogoro wa Kimataifa na wa Kienyeji

Rais Ruto amekiri kuwa mgogoro wa mafuta ni wa kimataifa unaosababishwa na mivutano ya kijiografia Mashariki ya Kati, na sio suala la Kenya pekee.

 Waandalizi na waandamano wanaonekana kuelewa hili, lakini wanahoji kuwa serikali haijafanya vya kutosha "kuwapunguzia" wananchi makali ya mivutano hii ya kimataifa, 

Katika makala hii sisi tunadhani ifike mahali serikali ipewe muda hasa miezi mitatu kisha tathimini ifanyike kwa kuzingatia ahadi zilizotolewa na Serikali.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpe.

Post a Comment

Previous Post Next Post