Chombo Cha Artemis II kilichosafiri Mwezini kwa muda siku kumi kiliwabeba wanaamga Reid Wiseman, Victor Glover, Christina Koch (Wamarekani/NASA), na Jeremy Hansen (Mkanada/CSA).
Je, Safari Yao ikuwaje?
Chombo hicho kilisafiri kwa siku siku (10) kuzunguka Mwezi, kikipita mbali zaidi kuliko mwanadamu yeyote alipowahi kufika tangu 1972.
Safari ya kurudi ikuwaje?
Kurudi duniani na kuingia angahewa ya Dunia (re-entry) ni sehemu hatari zaidi, ikihusisha nyuzi joto kali sana kiasi cha 5,000°F, kulingana na kasi ya 25,000 mph. ya chombo hicho.
Kukatika/Split Up:
Inasemekana chombo hicho kilisafiri huku kikimeguka na kupunguza hatua kwa hatua.hasa moduli ya huduma ndio hukatioa na kumeguka kutoka kwenye Ile moduli ya wanaanga. (Service Module) hutengana na moduli ya wanaanga (Crew Module) kabla ya kutua. Hii inaratibiwa na kompyuta/wanadunia.
Maisha ya wahanga ndani ya Orion
Wanaanga walikula na kunywa, na walitumia vyoo maalum vilivyofungamanishwa nao, Hawakuweza kutembea kama kwenye ndege kwani chombo ni kidogo na wamefungwa.
Kwa nini Kilitua Baharini:
Chombo kinatua baharini kwa sababu maji ni laini kuliko nchi kavu. Kimeundwa bila milango ya kawaida ili kuzuia hewa kutoka, hivyo wataalamu wa majini wanaosubiria kukipokea ndo (Navy) hufungua chombo hicho baada ya kutua.
Wahusika wa Artemis II walirudi salama Duniani mnamo Aprili 11, 2026, baada ya safari ya siku 10 kuzunguka Mwezi na kutua kwenye Bahari ya Pasifiki.
Kwa nini ilienda Mwezini?
Ilikuwa ni safari ya majaribio ya kwanza yenye binadamu (crewed test flight) ili kuthibitisha mifumo ya chombo cha Orion, kuwezesha kutua kwa mwezi siku zijazo (Artemis III/IV), na kuandaa safari za kwenda Mirihi (Mars).
Wahusika walinusurikaje ndani ya kapsuli?
Walinusurika kwa kutumia mfumo wa Life Support System uliopo ndani ya chombo cha Orion, unaosafisha hewa ya kaboni dioksidi, kusambaza oksijeni, na kudhibiti halijoto.
Je, Walichukua mitungi ya oksijeni?
Ndiyo, mfumo huo unahifadhi oksijeni katika matangi yenye shinikizo kubwa.
Je, wahusika walifunuliwa na mazingira ya nje ya mwezi?
Hapana. Wahusika walibaki salama kabisa ndani ya kapsuli ya Orion iliyofungwa (pressurized). Hawakufunuliwa na anga ya nje ya mwezi; kapsuli iliwalinda dhidi ya utupu (vacuum) na mionzi ya anga.
Ama kwa hakika Dunia imepiga hatua kubwa katika sayansi ya utaalamu wa anga za juu.
