#Viongozi wa upinzani nchini Kenya wameungana pamoja kumtuhumu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya ndani, Raymond Omollo kwa kufadhili Magenge ya Wahuni/Majambazi wanaowalenga viongozi wa kisiasa.Akizungumza na waandishi wa habari leo Tar 11, Aprili,2026, muda mfupi baada ya Seneta wa Vigiga Godfrey Osotsi aliyevamiwa na kujeruhiwa na Majambazi, Edwin Sifuna amejiunga na Wanasiasa wengine, Babu Owino pamoja na Viongozi wengine wa upinzani ambao wamempatia Katibu huyo wa Wizara ya Mambo ya ndani kipindi Cha siku (14) awe amejiuzuru.
Hata hivyo Edwin Sifuna hakudokeza ni hatua zipi ambazo watazichukua endapo takwa lao halitafanyiwa kazi. Katika kipindi Cha kati ya Tar 9-11, Aprili 2026, Wanasiasa wa mlengo wa Linda Mwananchi wamekuwa wakitoa madai ya Raymond Omollo kuhusika na kufadhili wa magenge ya Wahuni kwa lengo la kuwadhuru. Mwanzoni madai hayo yakitolewa na Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino hata kabla ya tukio la kuvamiwa kwa Godfrey Osotsi.
Babu Owino alidai kwa mara ya kwanza mnamo Februari 22, 2026,kwenye runinga ya Citizen kwenye mahojiano na Jeff Koinange, kwamba Raymond Omollo alifadhili vijana (goons) zaidi ya 200 wenye mapanga kuwashambulia yeye na Edwin Sifuna katika Uwanja wa Ndege wa Kisumu. kwenye safari Yao ya kutoka magharibi mwa Kenya waliokuwa wamekwenda kufanya mikutano ya Kisiasa.
Babu Owino alirudia madai hayo mnamo Februari 23, 2026 (KTN), Aprili 9, 2026 (baada ya shambulio la Seneta Osotsi), na Aprili 10-11, 2026, akidai Omollo anatumia vijana hao kudhuru wapinzani wa serikali. Aliongeza kwamba anao ushahidi wa kudhibitisha madai yake.
Tarehe 10-11 Aprili, 2026, Raymond Omollo alijibu tuhuma hizi kwa kukataa madai hayo, akisema viongozi hao wanatumia "reverse psychology" kumaanisha madai hayo hayo yalikuwa kinyume chake, na akahimiza polisi kuchunguza uhalifu badala ya siasa.
Aidha Waziri wa mambo ya ndani Kipchumba Murkomeni Mnamo Aprili 10, 2026, alimtetea Omollo, na kuushutumu upinzani kwa kuzunguka na na wahuni kisha kuitupia lawama serikali huku akiamuru polisi kuwakamata wote wanaohusika.K wa lugha nyingine ilionekana kana kwamba ni swala kurushiaana mpira kati ya serikali na wapinzani.
Tarehe 9 April 2026, mlengo mwingine wa upinzani unaohusisha kundi la Rigathi Gachagua, Fred Matiangi, Eugine Wamalwa na Kalonzo Musyoka nao waliungana na wale wa Linda Mwananchi kuunga mkono madai ya kuhusika kwa Raymond Omollo kufadhili Wahuni na Majambazi. Wakiwa kwenye mkutano wa siasa huko machakosi miongoni mwao Kalonzo Musyoka alisema haikutosha kuwakamata watuhumiwa watatu (3) huko kisumu na kumwacha Mhuni/ Jambazi mkubwa ambaye ni Raymond Omollo.
Awali taarifa zilisema Polisi waliwakama watuhumiwa watatu(3) mjini kisumu ambao wanahusishwa na tukio la kuvamiwa kwa Seneta wa Vigiga.
Hata hivo leo Tar 11 aprili, 2026 baada kutoka hospitali alipokuwa akipata matibabu, Seneta wa Vigiga Godfrey Osotsi amesema kwamba madai ya kuhusika kwa Raymond Omollo kufadhili uvamizi dhidi yake ni kweli na anao ushahidi.
Haijulikani matuo haya yataendelea hadi lini au endapo madai yanayotolewa na Wanasiasa wa upinzani yana ukweli kiasi gani. Kutokana na kukiri kwamba wanao ushahidi (Babu Owino) kwa mujibu wa Maelezo yao, na (Godfrey Osotsi) mara baada kutoka hospitali, huenda wakafungua mashataka rasmi dhidi ya Raymond Omollo. Tofauti na hivyo kwa sasa wametoa msimamo wao wa kumtaka ajiuzuru ndani ya siku 14. Ni swala la kusubiri.
