#WANAFUNZI WATUHUMIWA MKASA WA MOTO UTUMISHI GIRLS KUACHIWA HURU

Mwanasheria maarufu nchini Kenya, Danstan Omari amesena kwamba huenda Wanafunzi wanaokabiliwa na kosa la kuchoma na kutekeleza Bweni la shule

Utumishi Girls wakaaishiwa huru endapo mwendesha mashtaka atategemea ushahidi kwa kanda za CCTV kama ushahidi wa msingi kwenye kesi hiyo.

 Katika Maelezo ya Wakiri Omari mnamo Juni 2, 2026, ushahidi wa picha za CCTV ni batili na haukubaliki Kisheria kwa Sababu  umepatikana kinyume cha sheria, kuweka kamera za CCTV ndani ya bweni la wanafunzi wa kike kunakiuka uhuru wa faragha wa wanafunzi. 

Wakiri Omari aliongeza kusema kwamba kifungu Cha 31 Cha Sheria ya haki za msingi kwenye katiba ya kenya kinaruhusu uhuru wa faragha kwa kila Raia wa Kenya na kwamba Kamera zile za CCTV ziliwekwa ndani ya bweni wanamolala wanafunzi.

Kwa maana nyingine ili wahukumiwe wanafunzi wale labda uwepo ushahidi mwingine wa Polisi unaoweza kutumika kama vile ripoti za wakemia wakuu wa serikali kubaini iwapo kemikali zozote zilitumika kuanzisha moto huo, ushahidi wa mashahidi (wanafunzi wengine au walimu na watumishi wengine), na uchambuzi wa njia zinginezo.

Hatima ya kesi hiyo ya wasichana waliochoma bweni la Shule ya Utumishi Girls bado inasubiriwa huku wanafunzi wanane wakisalia rumande kwa siku 21 baada ya Kesi hiyo kutajwa tarehe 2 Juni, 2026, kwenye Mahakama ya Naivasha.  Wanafunzi hao wanakabiliwa na kosa la kula njama na kupanga kutekeleza kwa moto bweni la Shule ya wasichana ya Utumishi Girls, na kusababisha  vifo vya wanafunzi wenzao 16 wakiwemo na majeruhi 79 kwenye tukio hilo.


Post a Comment

Previous Post Next Post