#WINGU LA MAANDAMANO LATANDA KENYA KUPINGA KUINGIZWA NCHINI HUMO WAMAREKANI WENYE VIRUSI VYA EBOLA

 #Kuna uwezekano mkubwa wa kutokea Maandamano makubwa hivi karibuni kote nchini Kenya Kupinga kuingizwa au

kuletwa kwa wamarekani wanaougua ugonjwa wa Ebola au wenye dalili za maambukizi ya ugonjwa huo kutoka jamhurinya DRC Congo. Hii ni baada ya Serikali kusisitiza Kwamba uanzishwaji au ujenzi wa kituo Cha karantini kinachojengwa eneo la Kambi ya Jeshi ya Laikipia hautasitishwa.

Kauli hii ya Serikali ya Kenya inakuja licha kuwepo zuio la mahakama kuhusiana na mpango huo na kufanyika kwa  Maandamano Laikipia Jumatatu tarehe 1 Mwezi juni 2026 kupinga ujenzi wa kituo Cha karantini cha wagonjwa wa Ebola ambapo watu wawili walipigiwa risasi na kuuawa kwenye maandamano hayo.

1) Maelezo ya Aden Duale kwenye Bunge la Kenya:

Akiongea kwenye Bunge la Kenya  Jumatano tarehe 3 Juni 2026, Waziri wa Afya wa Kenya Aden Duale, alijipiga kifua na kusema kwamba hakuna kitakachoizuia Serikali kuendelea na ujenzi wa kituo Cha karantini cha wagonjwa wa Ebola huko Laikipia -- Nanyuki. Duale aliyasema hayo pindi akijibu maswali na hoja za Wabunge Kuhusu mpango mzima wa maandalizi ya Serikali Kuhusu mpasuko wa Ebola endapo Janga hilo litasambaa hadi nchini humo. Katika maelezo yake.aliongeza kusema Kwamba Kituo Cha karantini cha Ebola litakuwa miongoni mwa vituo 23 (ambavyo hakuvitaja) vya Ebola vinavyoandaliwa kote nchini Kenya.

#2.) Hoja ya Msingi ambayo Serikali ya Kenya Inakwepa kujibu:

Ni vema ieleweke vema kwamba hakuna mkenya yeyote anayepinga kuanzishwa Kwa vituo vya karantini kwa ajili maandalizi na tadhadhari kwa ajili ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, kinachogomba hapa ni makubaliano ya Serikali ya Kenya na Marekani kuhusu kuwaleta nchini Kenya Wamarekani wanaougua ugonjwa huo au wenye dalili za maambukizi ya ugonjwa huo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuja kutibiwa nchini Kenya. Hoja hii ndo chanzo cha mgogoro kati ya serikali na wananchi, Asasi za Kiraia na Wanaharakati.

#3.) Kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio:

Mbaya zaidi ni pale ambapo Serikali ya Marekani imekataa wazi kutoruhusu mgonjwa yeyote wa Ebola kuingia nchini mwao. Kwa maana nyingine, Serikali ya Marekani inataka kutumia nchi zingine kama kinga au dampo la kutibia Raia wa nchi hiyo wanaougua ugonjwa huo nje ya Marekani hadi watakapokuwa salama kurudi nchini mwao.

Mnamo Tarehe 27, Mei, 2026, Waziri mwenye dhamana ya maswala ya nje ya Marekani, Marco Rubio alisema kwenye kikao rasmi Cha Baraza la Mawaziri Ikulu ya Marekani 'White House' kwamba Marekani haitaruhu mgonjwa yeyote wa Ebola kuingia nchini humo, na kusisitiza Kwamba kipaumbele Cha Marekani ilikuwa ni kuhakikisha Usalama wa Wamarekani. Aliongeza kwamba Serikali ya Marekani imefanya mazungumzo na Serikali ya Kenya ili Wamarekani wanaougua ugonjwa huo au wenye dalili za maambukizi ya ugonjwa huo watapelekwa nchini Kenya.

#4.) Maandamano ya Laikipia na Hoja za Wananchi:

 Tarehe na Sehemu: 

Jumatatu, Juni 1, 2026, maeneo ya Nanyuki (Kaunti ya Laikipia) na baadaye wanaharakati wakaandamana jijini Nairobi.

Dondoo na Hoja:

 Mamia ya wananchi na wanaharakati waliingia mitaani wakipinga vikali mpango wa kuanzisha karantini ya wagonjwa wa Ebola katika Kambi ya Jeshi la Anga ya Laikipia. Walitaka kujua usalama wa jamii zinazozunguka kambi hiyo endapo virusi vitaenea, wakidai hawakushirikishwa katika uamuzi huo wa siri. 

Maandamano hayo yalisababisha ghasia zilizoripotiwa kuua watu wawili. Ubalozi wa Marekani ulitoa tahadhari ya usalama kwa raia wake.

5.) Kesi iliyofunguliwa na Katiba Institute:

Tarehe na Sehemu: Mei 28, 2026, katika Mahakama Kuu jijini Nairobi.

Dondoo na Hoja: Taasisi ya Katiba Institute, ikishirikiana na Chama cha Wanasheria Nchini (LSK), iliwasilisha kesi ya dharura kupinga mpango wa serikali na Marekani. 

Hoja zao zilieleza kuwa mpango huo unaleta hatari kubwa kwa afya ya umma, unakiuka utawala wa kikatiba kutokana na ukosefu wa ushirikisha umma, na unafanywa kwa siri bila uwazi. 

6.) Zuio la Mahakama:

Mei 29, 2026, Mahakama Kuu ilitoa amri ya muda ya kusitisha ujenzi na uingizaji wa wageni walioathirika na Ebola hadi kesi hiyo isikilizwe na kuamuliwa.

7.) Chama cha Madaktari na Wauguzi (KMPDU na KMA)Tarehe na Sehemu: Press iliyofanyika Nairobi mwishoni mwa Mei 2026.  

Dondoo na Hoja: 

Vyama vya madaktari viliukosoa mpango huo vikisema Kenya haiko tayari wala haina uwezo wa kiutabibu na miundombinu ya kukabiliana na Ebola. Walipinga vikali kuwafanya wauguzi na madaktari wa Kenya kuwa wahudumu wa kwanza wa wageni walioambukizwa ilhali nchi yao haina vifaa vya kutosha. Walitoa onyo la mgomo wa kitaifa.

8.) Maelezo ya Aden Duale na Hoja za Serikali: 

Tarehe na Sehemu: Mahojiano kwenye kipindi cha Citizen Weekend, Citizen TV, usiku wa Jumamosi, Mei 30, 2026.

Dondoo na Hoja: 

Waziri wa Afya Aden Duale alitetea mpango huo akisisitiza kuwa kituo hicho kitasimamiwa na wanajeshi wa Kenya (KDF) pamoja na wataalamu wa Marekani. Alionya wanasiasa wasilifanye suala hili la afya kuwa la kisiasa. Alifafanua kuwa kituo cha Laikipia ni moja kati ya vituo 11 vya karantini vinavyojengwa nchini kama tahadhari, na kimesanifiwa kuhudumia wote (Wakenya na Wamarekani).

9.) Maelezo na Msimamo wa Rais William Ruto: 

Tarehe na Sehemu: Rais Ruto alizungumza kwa kina na vyombo vya habari akitetea mpango huo mnamo Juni 2, 2026.

Dondoo na Hoja:

 Rais Ruto alikiri kwamba aliidhinisha kituo hicho baada ya ombi maalum kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump. Alitetea kituo hicho kama sehemu ya makubaliano na mshirika mkuu anayeisaidia Kenya. 

Rais alifafanua kuwa kituo cha Laikipia sio cha kipekee, kwani Kenya tayari ina vituo zaidi ya 20 vya magonjwa ya kuambukiza nchini kote, na alikosoa vikali siasa zilizopigwa kuhusu mradi huo.

10.) Harufu ya Mgomo:

Endapo serikali itapuuza maagizo ya mahakama, malalamiko ya wananchi, na madai ya vyama vya afya na Asasi za Kiraia, ni dhahiri kuwa kutashuhudiwa Mgomo Mkubwa kote nchini utakaohusisha Wananchi, Wanaharakati, vyama vya Asasi za Kiraia na Wahudumu wa Afya.

 Hali hii inajengeka kutokana na sababu zifuatazo:

Ushirikiano wa Kimkakati:

 Chama cha Madaktari (KMPDU) tayari kimetishia kuchukua hatua za kususia kazi. Hatua hii itapata uungwaji mkono wa wanasiasa wa upinzani na asasi za kiraia. 

Hofu Kuu ya Jamii:

 Wananchi wameonyesha ghadhabu kuu kwa swala hili, na hatua ya kuendelea na mradi huu kinyume cha matakwa ya Kisheria, hasa kitendo cha Serikali ya sasa kuonyesha Wazi Kutanguliza Maslahi ya Wamarekani kuliko Wakenya kisa tu kwamba Wamepewa Mabilioni ya pesa. Hii ndo chachu ya maandamano ambayo hayatazuilika.

Post a Comment

Previous Post Next Post