
Tunaichambua taarifa hiyo kama ifuatavyo:
1. Wakenya Kulipa Fadhila:
Akihojiwa na Mwandishi Kylie Kumalo kutoka shirika la utangazaji la SABC News. baada ya kuulizwa Swali la Msingi:
Mwandishi huyo alimuuliza Rais Ruto kuhusu hali ya sintofahamu na ukosoaji mkubwa uliokuwepo nchini Kenya kufuatia makubaliano ya kuanzisha kituo cha kuweka karantini (kwa ajili ya Wamarekani watakaokumbwa na Ebola) nchini Kenya, na akataka kujua majibu yake ya haraka kuhusu ghadhabu ya Wakenya:
Majibu ya Rais Ruto:
Rais Ruto alieleza kuwa Ebola ni janga la kimataifa ambalo haliepukiki na halijafungiwa sehemu moja. Alifafanua wazi kuwa hadi wakati huo hakukuwa na kisa hata kimoja cha Ebola kilichoripotiwa nchini Kenya. Aliongeza kuwa kutokana na Kenya kuwa na maelfu ya wananchi na askari katika eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako kulikuwa na mlipuko mkubwa hatua ya kujitayarisha kwa lolote lililokuwa likijiri ilikuwa ni jambo la uwajibikaji.
Mikakati:
Alisema Kenya ilikuwa imechukua udhibiti wa vituo vyake vyote vya kuingilia na ilikuwa ikipima maelfu ya watu kila siku kutoka maeneo hayo. Hata hivyo Ruto alisema kwamba Kenya imekuwa ikipokea msaada kutoka kwa Marekani kwa takriban miongo miwili ni ilikuwa mwafaka kurudishwa fadhila kwa wamarekani.
Ombi la Marekani malipo ya Fadhila:
Ruto Alikiri kuwa Serikali ya Marekani iliomba kuwasitiri wafanyazi wake wanaohudumu kwenye ukanda afrika hasa DRC Congo kutibiwa kwenye kituo cha karantini ya Kenya na isingekuwa busara kukataa Ombi hilo kwa vile ni kinyume na ubinadamu na kuongeza hiyo ni fursa ya kenya kulipa fadhila. Alieleza kuwa uamuzi huo unaakisi shukrani kwa msaada wa Marekani katika sekta ya afya kwa zaidi ya miongo miwili.
Hoja ya Msingi:
Hata hivyo, wengi wanaopinga wanahoji ni kwa nini Kenya ilazimike kuweka maisha ya wananchi wake hatarini ili kulipa fadhila kwa misaada inayopewa na Marekani!?
2. Maelezo ya Awali:
Serikali ya Marekani iliahidi kutoa dola za Kimarekani milioni 13.5 (sawa na takriban Ksh bilioni 1.74 au TZS bilioni 35.5) kusaidia maandalizi ya dharura ya Ebola nchini Kenya, ikiwemo ujenzi wa kituo hicho katika Kambi ya Jeshi la Anga ya Laikipia.
3. Msimamo wa Serikali:
Rais Ruto alisema wananchi wanaopinga mpango huo na kufanya migomo ni kwa Sababu ya kutokuwa na taarifa. Mpango huo umezua maandamano na taharuki kubwa kutoka kwa wataalamu wa afya, wanaharakati, na wananchi wanaohoji uhalali wa Kenya kuwahudumia wagonjwa wa kigeni wenye maambukizi hatari kutoka DRC.
4. Zuio la mahakama:
Mahakama Kuu nchini Kenya ilitoa amri ya kusitisha ujenzi na shughuli zote katika kituo hicho hadi kesi ya msingi isikilizwe.
Licha ya amri hizo na upinzani mkali, Waziri wa Afya Aden Duale alisisitiza mbele ya Bunge kuwa serikali haitasitisha ujenzi, akiita maandamano hayo kuwa ya "watu wachache" na akatangaza wazi kuwa ujenzi wa kituo hicho cha karantini ya Ebola hautahitaji ushirikishwaji wa wananchi (public participation).
5. Utata wa Vituo 23 vya Karantini:
Serikali KUPITIA Rais Ruto na Waziri wake Duale imetaja uwepo wa vituo vingine vya karantini zaidi ya 20 nchini. Hata hivyo, kuna upinzani mkali na ukosoaji kwamba maeneo halisi na uwezo wa vituo vingine 23 havikujulikani vilipo Wala kutajwa wazi.
Ukweli kwamba kambi ya jeshi la Laikipia ndiyo kitovu kikuu kinachoonekana kupokea vifaa na wataalamu kutoka Marekani kumezua sintofahamu kubwa.
6. Hoja za Wakenya na Usiri wa Mradi:
Wakenya wengi hawapingi kuwepo kwa maandalizi ya kujihami na Ebola, kwani ni dharura ya kiafya ya kimataifa.
Upinzani unatokana na uamuzi wa makusudi wa kuruhusu wagonjwa au watu walio katika hatari ya Ebola kutoka nchi jirani (DRC) kuletwa nchini Kenya, badala ya kutengwa kwenye nchi zao au kusafirishwa moja kwa moja hadi Marekani.
7. Usiri wa Mradi na Ukosefu wa Uwazi:
Katika mahojiano kwenye Kipindi cha JKL Cha Runinga ya Citizen, tarehe 3 juni 2026, kati ya Waziri Aden Duale na Mtangazaji Jeff Koinange, Waziri huyo wa Afya wa Kenya alikataa kuruhusu Vyombo vya habari kutembelea eneo la Laikipia kinapojengwa kituo hicho Cha karantini ya wamarekani na badala yake kumtaka aende na timu yake Hospitali ya Taifa ya Kenyatta.
8. Kauli za Viongozi na Tofauti za Kimisimamo
Rais Ruto alitetea mpango huo na kusisitiza kuwa maandamano na upinzani unatokana na ukosefu wa uelewa wa kina kuhusu mpango huo miongoni mwa wananchi. Je, ni jukumu la nani kuhabarisha Umma wa Wakenya?
Kwa upande mwingine, lugha dharau na kiburi ya Aden Duale:
I) Waziri Aden Duale alitamka wazi Bungeni kwamba mpango wa kuanzisha kituo Cha karantini ya a Laikipia hautasitishwa.
II) Dharau Kwamba maandamano ya Watu watatu, wanne au kumi si hoja kuzuia mpango huo.
III) Aden Duale na Rais Ruto wote wanajua kwamba Kuna zuio la mahakama lakini wanakaidi kwa makusudi.
IV) Maandamano ya Laikipia yalisababisha vifo vya watu wawili (2). Hii Ina maana Ebola tayari imeshaanza kuja wananchi hata kabla ya kuingia Kenya.
V) Waziri alikataa kuruhusu Vyombo vya habari kwenda eneo la tukio Kule Laikipia ili kuandaa makala maalumu.
Haya ndo mambo yanayozua hoja na maswali kutoka kwa Wananchi wa kenya ambayo ikekataa kushirikisha Umma.
Toa maoni yako....