#SIMBA ARATI ALIPA KISASI CHA KIPIGO KWA MCA ALIYEHAMA KAMBI YAKE

 Gavana wa Kisii Simba Arati anamulikwa na Jamii ya Kisii kwa kufadhili tukio la

kuvamiwa kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa MCA wa Ward ya eneo la Ichuni, Wycliffe Siocha maarufu kama 'Embande' 

Siocha alishambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana mnamo Juni 4-5, 2026 alipokuwa akihudumia gari lake kwenye gereji karibu na Uwanja wa Gusii mjini Kisii na anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Hema mjini Kisii.

#KUHUSIKA KWA SIMBA ARATI:

Upekuzi wetu umebaini kuwepo kwa taarifa ambazo hatujazithibitisha tunazofatilia zinazomhusisha Gavana Simba Arati kufadhili Genge la wahuni kwenda kumvamia na kumuumiza Siocha kwa kile kinachosadikiwa kuwa kisasi cha Kisiasa baada ya MCA huyo kutangaza kuhama kambi ya Simba Arati na Kujiunga na mlengo wa Jubilee wa Ezekiel Machogu ambaye anamuunga mkono na Dr Fred Matiang'i.

#UPINZANI KUTOKA KWA EZEKIEL MACHOGU:

 Tukio hili linakuja kukiwa na badiliko la upepo wa siasa za Kisii ambapo Arati anakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu. Machogu ameonyesha nia ya kupambana na Simba Arati kwa nafasi Gavana kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2027.

Ezekiel Machogu pamoja na viongozi wengine walijitokeza kumtembelea MCA Siocha hospitalini na kuwasilisha malalamiko rasmi kwa polisi wakitaka uchunguzi wa kina ufanyike Kuhusu tukio la kushambuliwa na kuumizwa kwa Siocha.

UHASAMA KATI YA ARATI NA OSORO:

 Gavana Simba Arati amekuwa na uhasama wa Kisiasa wa muda mrefu na Mbunge wa South Mugirango, Silvanus Osoro, kuongezeka kwa kundi lingine la Ezekiel Machogu kunamfanya kuwa na makundi mawili kinzani yanayomweka kwenye mizani ya siasa za Kisii huku kukiwepo na dalili za kutoridhishwa kwa Jami ya kisii kwa utendaji wake.  Hata hivyo, hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kwamba kiongozi huyo wa wengi Bungeni amehusika katika tukio la hivi punde na isitoshe, hakujakuwa na usahasama wowote kati ya Osoro na Siocha au na Ezekiel Machogu.


.



Post a Comment

Previous Post Next Post