#VIGOGO WA KAUNTI ZA KENYA NI UFISADI MTUPU

Maafisa wa Idara huru ya Serikali ya Kenya(EACC) inayoshughulikia maadili ya watumishi wa umma na kupambana na rushwa na ufisadi nchini humo

wamemkamata Afisa Mkuu wa Mipango na Maendeleo ya Miji wa Kaunti ya Nairobi Patrick Analo, akiwa na rundo la pesa zaidi ya Ksh 65 Milioni Nyumbani kwa Afisa hiyo eneo la Syokimau Jijini Nairobi.

Fedha zimekutikana kwenye vyumba mbalimbali kwenye Nyumba ya Mtumishi huyo wa Kaunti ya Jiji la Nairobi ambapo taarifa zinasema pesa zingine zilifichwa kwenye Magari yaliyokuwa yameegeshwa nje ya Nyumba yake.

Kwa mujibu wa Vyombo vya habari vya kenya ikiwemo runinga za Citizen na Nation, fedha hizo zinaaminika kupatikana kwa njia ya rushwa. Maafisa wa EACC wameeleza kuendelea kuwasaka maafisa wengine wa Kaunti ya Nairobi ambao wanaaminika kuwa sehemu ya mtandao wa mtuhumiwa aliyekamatwa na fedha ambayo haina maelezo sahihi ya chanzo chake.

Tukio hili ni tone la maji baharini kwani inasadikiwa Kwamba maafisa wa Serikali kuu na wale wa Kaunti zote nchini Kenya wanahusika na rushwa za namna moja ama nyingine. Inasikitisha Kwamba wakati Wananchi wa kawaida wa Kenya wanaishi chini ya kivuli cha lindi la umasikini wa kutomudu japo mulo wa siku, na hasa gharama za juu za maisha, baadhi ya watumishi vigogo wa Kaunti wanatafari nini wazifanyie pesa walizokusanya kwa rushwa na ufisadi, wakishindwa wazitumze wapi? Au  wazipangie matumizi gani? 

Hiyo ndo picha halisi ya utendaji kwenye kaunti za kenya, hicho ni kisa kimoja tu, laiti ungefunuliwa picha ya jumla ya kinachofanyika kwenye ofisi hizi za umma ungetamani ardhi ipasuke ikufukie, usione Wala kusikia. Watu wanapiga Hela kiasi kwamba hata kuzipangia matumizi wanashindwa. Hiyo ni Kenya.

Post a Comment

Previous Post Next Post