#1. Kwanini watoa huduma hukata faida (ada ya mkopo) kabla ya matumizi?Makampuni ya simu kama vile Safaricom na Airtel hutoza ada ya mkopo
(kama vile \(10\%\)) wakati wa kutoa mkopo wa Okoa Jahazi au huduma kama Fuliza.Sababu za kibiashara:
Hii inafanyika ili kampuni ijihakikishe faida yake papo hapo kwa kuwa huduma inatolewa bila dhamana licha ya kwamba mteja huyo amejisajiri kutumia mtandao huo.
Usimamizi wa Hatari:
Ukatwaji huu wa moja kwa moja hauzinhatii ukweli kwamba Kampuni hizo hazitoi vifurishi vinaendana na salio linalobaki: mfano, ukikopa Ksh 10 itapewa 9\=, ukikopa Ksh 20 utapewa 18/= na ukikopa Ksh 50 utapewa 45/=. Ajabu ni kwamba hakuna kirufushi Cha data au muda wa maongezi unachoweza kupata kwa salio linalobaki ama vinginevyo ukope tena endapo kiwango Cha kukopa kinaruhusu.
Matokeo yake ni kulimbikiza deni na mara nyingi inambidi mteja apige simu bila kuunga kifurushi.
2. Huu ni Mfumo wa Kibepari;
Kampuni hizi za kenya kimsingi halipaswi kuwa WATOA huduma, ilipaswa ziwe kwenye kundi la viwanda vinavyozalisha bidhaa. Hii ni kwa Sababu wao hawataki kujua kama salio linalobaki linatosha uunge bando au hapana ilimradi wamechukua chao mapema.
Unyanyasaji na Uonevu:
Katika nchi nyingi za afrika ikiwemo afrika Mashariki, wananchi hutumika njia ya kuunga bando au vifurishi vya data au muda wa maongezi ili kuepuka gharama kubwa ya kupiga simu tofauti na ilivyo kwa jinsi zilizoendelea ambapo wao hukatwa Dola, sasa tunapokuwa na Kampuni ambazo hazianhalii maslahi ya wateja wao ni sawa na unyanyasaji kwa wateja.
Ulazima/ Umuhimu wa huduma:
Huduma za Mawasiliano ni kama dawa. Mgonjwa akiugua lazima aende hospitali ambapo atapimwa uzito, sijui presha, sukari nk ilimradi bili iongezeke. Kwenye mawasilianonpia ndivyo ilivyo na hasa kutokana na ukiritimba uliopo hususan kwa kampuni ya safaricom ya Kenya, mteja hana chaguo lingine na hana pa kulalamika. Ndo wahenga wakisema Dunia hadaa ulimwengu shujaa. Mteja mwenye shida ni lazima atapiga simu japo muda huo Kuna mabwanyenye wamekaa sehemu wakihesabu faida kila sekunde kisa na maana wao ni wenye hisa ilimradi kufa kufaana.
UHALISIA:
Ukweli ni kwamba mtindo huu unaleta malalamiko ya wateja kuwa mfumo unaonekana kuwa kandamizaji.
Hali halisi:
Mfumo huu unaondoa urahisi wa mteja kujumuisha kiasi kilichobaki baada ya kukopa na kukatwa papo hapo inabidi kukopa tena pesa nyingine ili kununua kifurushi moja kwa moja au kupiga simu makavu.
Huu ni Unyanyasaji mkubwa sana wa kihuduma dhidi ya Ukweli wa Kibiashara: Kisheria na kibiashara, mikopo ya muda wa maongezi huchukuliwa kama huduma ya haraka ya dharura.
Hata hivyo, wateja wengi huona kama ni mtego au mfumo kandamizi pale wanapojikuta wanashindwa kufanya lolote na salio lao dogo.
Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA) imekuwa ikipokea malalamiko mengi ya namna hii yakitaka uwazi zaidi wa utozaji bili japo hakuna hata chembe ya hatua waliyowahi kuchukua kwa vile na wao pia ni sehemu ya mfumo huo wa kibwanyenye na wakandamizaji. Unaambiwa kesi ya nyani ukiipeleka kwa tumbili ni kupoteza muda.
Serikali kumiliki Hisa kwenye Kampuni za simu:
Hili ndilo donda ndugu linaloitafuna mifumo ya kampuni ya Kenya, hasa Safaricom. Serikali ya Kenya inapokuwa mmiliki wa hisa kwenye kampuni inayotoa huduma wananchi wakosa pa kusemea kwa sababu Ina WAJIBU wa kutatua kero au malalamiko ya wananchi ili kuboresha huduma. Tofauti na hapo Serikali ya Kenya ndo bwanyenye wa kwanza inaendelea kukomba faida lukuki na hata kulamba vidole, imeweka pamba masikioni. Haisikii Wala haiambiliki.
3. Njia Mbadala/Nafuu:
Mfano: Kwanini mteja anayekopa Ksh 50 asipewe taslimu na kurejesha Ksh 55 wakati wa kulipa badala ya kukatwa Ksh 5 mwanzoni kabla hajatumia?
Sababu tulizopata ni kwamba watoa huduma hutumia mfumo wa sasa kwa sababu kuu mbili:
Ukosefu wa Dhamana:
Mteja wa kulipia kabla (prepay) hana mkataba rasmi na kampuni ya simu. Kutoa kiasi chote kisha kulipisha faida baadaye kunaongeza hatari ya mteja kutolipa kabisa deni hilo.
Gharama za Mzunguko wa Fedha:
Kukata ada ya huduma (commission) kabla ya mwanzo kunaiwezesha kampuni kupata mtaji wa kujiendesha papo hapo.
4. Mifano ya Nchi Jirani:
Hapa tunaipigia mfano Tanzania:
Kwanini makampuni ya Tanzania yanatoa mkopo kamili na kukata deni likiwa na faida mteja anapoongeza salio?
Tofauti za kibiashara na mifumo ya kisheria au kiushindani ndizo zinazoleta utofauti huu baina ya nchi hizi.
Katika masoko mengine kama Tanzania, ushindani mkali wa kibiashara kati ya watoa huduma (kama Vodacom, Tigo, Airtel) huwalazimu kutoa masharti nafuu zaidi ili kuvutia na kubakiza wateja.
Mkakati wa soko la Kenya:
Nchini Kenya, kukiwa na soko lenye ushindani na uhitaji mkubwa, watoa huduma wana uwezo mkubwa wa kupanga viwango vya faida na masharti yao kulingana na sera zao za ndani ili kulinda uwekezaji wao mkubwa wa miundombinu.
Hapa ndipo inapokuja hoja ya Kenya kurusu uwekezaji wa makampuni mengine ya simu ili kuongeza ushindani ambao utapunguza gharama za Mawasiliano na data.
Lakini hili haliwezekani endapo serikali ya Kenya itaendelea kubaki kama mwenye hisa kwenye kampuni moja huku wananchi wakiumiza kwa gharama kubwa za Mawasiliano. Ifike sehemu sasa wananchi na bila shaka wale Wanasiasa wanaodai kulinda Mwananchi au wanaopania nyadhifa mbalimbali walione na walisemee hili swala kwa maslahi ya Umma.
5. Hitimisho:
Je, mitandao ya simu ya Kenya imejengwa kwa misingi ya kumkandamiza mteja?
Ni dhana ambayo wateja wengi wamekuwa nayo, lakini kiuhalisia:Hali halisi:
Mitandao ya simu ni wafanyabiashara wakubwa wanaolenga kutengeneza faida kubwa. Hivyo, wamebuni huduma hizi kama mikopo ya dharura yenye masharti yanayolinda maslahi yao ya kifedha badala ya huruma ya kijamii.
Mtazamo wa Kisheria:
Hata kama wateja wanahisi wanakamuliwa, mifumo hii hufuata sheria na kanuni zilizoidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA) kupitia mikataba ya kujiunga na huduma ambayo mteja huikubali wakati wa kununua laini. Lakini kwa hili ni vema tusimung'unua maneno, Mamlaka ya Mawasiliano Kenya ni muhilimi wa Serikali ambayo ni mwenye hisa kwenye baadhi ya kampuni za simu, sasa unatarajia itoe mkataba gani kwa mteja anayejiunga au kujisajiri na Kampuni ya simu? Na utashangaa kwamba hakuna mtu husoma maelezo Yale, kwa Sababu
i) Ni ya Kisheria,
ii) Yametengezwa kumbana mtumiaji,
iii) Yana lengo la kuilinda Kampuni,
iv) Ni malefu sana si rahisi mteja kukaa kuanza kuyasoma,
v) watu wengi wana uelewa mdogo,
vi) Hakuna chaguo lingine,hata kama hutaki utaenda wapi?
Lakini jiulize kama mteja anataka Mawasiliano na Kampuni hiyo ndo pekee iliyopo, afanyeje? Aache kuwasiliana?
Kila kampuni inajiendesha kibishara, na kwa kuwa mitandao inamilikiwa na Mashirika binafsi, misingi yake mikuu ni faida, ingawa masharti huweza kubadilishwa kulingana na ushindani wa soko au maelekezo ya serikali.
Toa maoni yako...
