Bunge la Kitaifa la Kenya limempitisha
Mswada wa Fedha wa mwaka 2026/27 kupitia kura ya tatu alasiri ya leo, Juni 18, 2026. Wabunge 122 waliunga mkono mswada huo huku 40 wakikataa, na sasa unasubiri kutiwa saini na Rais kuwa sheria kamili.Kuhusu bajeti yenyewe, makadirio ya matumizi ya KSh trilioni 4.8 kwa mwaka wa kifedha wa 2026/27 tayari yaliwasilishwa bungeni Juni 11, 2026 na Waziri wa Hazina John Mbadi. Mswada huu mpya umeondoa au kurekebisha baadhi ya kodi zilizokuwa zikilalamikiwa ili kupunguza mzigo kwa wananchi na wafanyabiashara.
Ushiriki wa Idadi Ndogo ya Wabunge:
Bunge la Kitaifa la Kenya lina jumla ya wabunge 349 (pamoja na Spika ambaye ni mwanachama wa ofisi anayefanya jumla kuu kuwa 350). Idadi ya wabunge waliopitisha mswada wa fedha wa mwaka 2026/2027 inaonekana kuwa ndogo ukilinhani na idadi juu ya Wabunge wote.
Katiba ya Kenya licha ya kutafusiriwa kuwa bora zaidi afrika haiweki kifungu kinachotaja theluthi ngapi ya Wabunge wanatakiwa kuwepo ukumbini kisheria kwa ila inaweka kiwango cha chini kabisa cha idadi ya wabunge (akidi au quorum) ili vikao na maamuzi ya kawaida yaendelee kuwa Wabunge hamsini tu (50).
Ni ajabu kubwa kwamba Katiba ya kenya inawaacha nje Wabunge 299 ambao si lazima wawepo bungeni pindi bunge linapopitisha maamuzi nyeti kama vile bajeti ya Taifa. Lakini Cha kushangaza zaidi ni kwamba wabunge hao watoro wanaopewa uhuru na katiba, licha ya kulipwa mishahara minono na marupurupu kibao kwa uwakilishi wa wananchi, utawaona huko nje kwenye majukwaa ya siasa au wengine katika safari za malipo nje ya nchi.
Inasikitisha kwamba wabunge 160 wanaweza kushiriki kupitisja bajeti ya nchi yenye idadi ya watu zaidi ya Milioni hamsini (50) huku wengine wakiwa wanakula Bata nje ya Bunge na kuwanyima uwakilishi wananchi waliowachagua.
Mchanganuo wa Idadi ya Wabunge Kwa mujibu wa Kifungu cha 97 cha Katiba ya Kenya, bunge linaundwa na wabunge 290 waliochaguliwa kutoka maeneo bunge, Wawakilishi wa kike 47 waliochaguliwa kutoka kaunti 12,Wabunge walioteuliwa kuwakilisha makundi maalum ni mbunge mmoja (1) Spika (mwanachama kwa wadhifa wake/ex-officio).
Sababu ya Idadi ya Kura Kuonekana Ndogo kura 120 za Ndio na 40 za Hapana Jumla ni 160 idadi hii ni halali kisheria kwa sababu mbili kuu:
Akidi ya Wabunge 50 tu:
Kuwepo kwa Akidi (Quorum) Wakati wa vikao vya kawaida vya bunge, si lazima wabunge wote 349 wawepo ukumbini. Sheria unahitaji kuwepo Wabunge hamsini tu ili vikao vya bunge viendelee.
Uamuzi kwa Wingi wa Kura (Simple Majority):
Kwa miswada ya kawaida kama Mswada wa Fedha, maamuzi yanatolewa kwa kuangalia wingi wa kura za wabunge waliopo na wanaopiga kura siku hiyo, mradi sheria ya akidi imetimizwa.
Kifungu cha 121 cha Katiba ya Kenya kinaelekeza kuwa Akidi ya Bunge la Kitaifa ni wabunge 50 Ikiwa bunge lina zaidi ya wabunge 50 ukumbini, lina uwezo kamili kisheria kuendesha vikao, kujadili, na kupitisha miswada.
Katika kikao Cha Bunge Cha tarehe 18 Juni 2026, jumla ya wabunge 160 walishiriki, idadi ambayo imepita mbali kiwango cha chini cha wabunge 50 kinachotakiwa na Katiba.
HitimishoBunge la Kitaifa lina jumla ya wabunge 349. Kura za wabunge 120 wa ndio na 40 wa hapana ni halali kabisa kwa sababu zimezidi kiwango cha chini cha wabunge 50 kinachohitajika kuendesha vikao na kufanya maamuzi bungeni kwa mujibu wa Kifungu cha 121 cha Katiba ya Kenya.
Maoni yako ni muhimu......
