Viongozi wa upinzani waongoza maandamano ya wanaharakati na familia za wahanga wa machafuko na vurugu za Finance Bill 2024.
Kumeshuhudiwa maandamano leo tarehe 18 Juni 2026, sehemu mbalimbali za Jiji la Nairobi yaliyofikia kilele chake kuelekea Jogoo House kwenye ofisi za Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja huko Jogoo House.
Maandamano haya ya leo yameandaliwa na makundi ya wanaharakati, vijana, na mashirika ya haki za binadamu yameelezewa kuwa na lengo la kumtaka Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja kutoka hakikisho la kufanyika maandamano ya kumbukumbu ya waathirika wa mswada wa fedha wa mwaka 2024.
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa waandamanaji wamejitokeza kwa wingi katika eneo la mji Nairobi CBD na baadaye kuelekea Jogoo House.
Viongozi Walioshiriki:
Maandamano hayo yamehusisha viongozi mbalimbali wa kisiasa na wanaharakati wa haki za binadamu, akiwemo:
David Maraga – aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kenya, akihimiza uwajibikaji na haki kwa wahanga
Martha Karua – wakili na kiongozi wa upinzani, akisisitiza haki za kiraia
James Orengo Gavana wa Siaya, mkosoaji wa matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji
Gitobu Imanyara – mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binadamu
Hussein Khalid Mkurugenzi wa Kituo Cha Vocal Africa, akiongoza ufuatiliaji wa haki za waathirika pamoja na makundi ya vijana wa Gen Z na mashirika mengine ya kiraia
Sababu:
Lengo kuu la maandamano haya kuomba ridhaa au uhakikisho wa kufanyika kwa maandamano ya kumbukumbu yanayotarajiwa tarehe 25 Juni 2026.
Kutaka siku ya tarehe 25 Juni 2026 iwe siku ya mapumuziko kwa ajili kuwakumbuka vijana wa GenZ waliopoteza maisha kutokana na ukatili wa polisi.
Kuzuia matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, maandamano ya 2024 yalipelekea vifo na majeruhi wengi, huku takwimu zikionyesha mamia ya walioathirika kote nchini .
Mapokezi na hatua za Serikali:
Viongozi wa wa Maandamano hayo wamepokelewa na kuruhusiwa kuingia ofisi za makao makuu ya polisi huku wafuasi wao wakizuiliwa kusalia nje.
Hata hivyo taarifa zinasema Kimsingi ombi la maandamano halijakataliwa kwa masharti ya kutofanya vurugunna uvunjifu wa amani. Aisha ombi la siku hiyo kuwa ya mapumuziko limekataliwa na serikali.
