#Hakuna kazi isiyokuwa na changamoto zake lakini lakini majaribu mengine
inataka moyo hasa pale huduma Inapogeuka Kuwa Mtihani wa Maadili.Katika dunia ya leo, vijana wengi wameamua kujiajiri kupitia kazi mbalimbali za halali ili kujipatia kipato cha kila siku. Miongoni mwa kazi hizo ni huduma za kutinda na kuosha kucha za wadada. Siku hizi akina dada wengi wametekwa na usasa, kwamba hawawezi kufanya usafi wa kucha zao hadi wakaoshwe na kutindwa ndo kisha zipakwe rangi. Si neno kwa vile urembo ni gharama. Wanawake wengi katika maeneo ya Mijini huenda kwa vijana wenye Salon au vibanda vya kufanya kazi hii ya urembo ya kuosha, kutinda na kupaka rangi kucha.
Hata hivyo, nyuma ya huduma hiyo inayolenga urembo na ustaarabu, kuna changamoto ambazo baadhi ya watoa huduma hukutana nazo. Miongoni mwa changamoto hizo ni majaribu yanayotokana na baadhi ya wateja wasiokuwa na mipaka ya maadili katika namna wanavyojihusisha na watoa huduma.
# Hesabu ya Mapaja ya wanawake:
Itoshe kusema hapa kwamba tatizo Si huduma inayotolewa na vijana hawa ila tabia za wateja wao. Si siri kwamba baadhi ya wakina dada hufika kwenye maeneo hayo wakiwa wamevaa mavazi mafupi kama sketi fupi au magauni yenye mipasuo kiasi cha kuacha sehemu za Miili yao wazi.
Wakati wa huduma, utamkuta dada kaweka mguu juu ya magoti ya kijana anayewahudumia huku sehemu za mapaja yao zikiwa wazi kabisa. Mbaya zaidi wanawake hawa wa Kisiasa hawatembei walah hata na khanga au kikosi Cha kujisitiri. Ndani ya mikoba Yao utakuta vitu kama simu,lip stick, kioo,vipodozi, pochi ya hela au funguo pamoja na vinginevyo. Hakuna khanga au Leso. Hii humfanya mtoa huduma kuishia kuhesabu mapaja ya wateja anaowahudumia.
Tatizo hili sio tu kwenye swala hili tunalojadili bali hata wanapokuwa kwenye vyombo vya usafiri mara nyingi hushindwa kujisitiri pale maungo Yao yanapobakinwazi kwa vinguo vyao vifupi wanavyovaa.
Kwa kijana ambaye kazi yake ni kuhudumia wateja kwa weledi, hali hiyo inaweza kuwa mtihani mkubwa wa kujidhibiti. Kazi ambayo ilipaswa kuwa ya kawaida ghafla hujikuta imezungukwa na mazingira yanayoweza kuvuruga umakini, heshima na hata maadili ya kazi.
# Hitimisho
Jamii yenye maadili hujengwa na watu wanaoheshimu utu wa wenzao na kutambua mipaka ya mazingira wanayokuwemo. Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha kwamba sehemu za kazi zinabaki kuwa maeneo ya huduma, si maeneo ya kuibua vishawishi visivyo vya lazima. Kinachoshangaza sana ni kwamba wanawake wenye tabia hizi si kwamba hukoswa nguo nzuri zinazositiri miili Yao madukani au sokoni, bali hufanya hivyo kwa makusudi mazima ya mioyoni na nafsi zao.
Nasaha:
Wateja waheshimu mazingira ya kazi kwa kuvaa kwa staha na kuzingatia maadili ya jamii, huku watoa huduma wakidumisha weledi, nidhamu na kujitambua katika kazi zao. Maadili mema ni msingi wa heshima, utu na maendeleo ya jamii nzima.
