#AFRIKA BADO INATAFUNWA NA UKOLONI WA WATAWALA WA KIIMLA

 Baada ya  machafuko ya Tanzania sasa ni somalia. Machafuko yaliyozuka nchini

Somalia hivi majuzi mnamo Tarehe 3-5 mwezi Juni 2026 yaliyasababishwa na mvutano mkali wa kisiasa na maandamano tofauti kidogo tunna iliyokuwa nchini Tanzania japo yote yanahusika na Wala la katiba na misingi ya Uongozi.

#1. Viongozi walioongeza muda na madai ya upinzaniRais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongeza muda wake wa uongozi. Upinzani unadai kuwa kuongezwa kwa muda wa mwaka mmoja hadi 2027 ni kinyume cha katiba. Upinzani unasisitiza kuwa muda rasmi wa Rais uliisha mwezi Mei 2026. Upinzani unapinga marekebisho ya katiba yaliyofanywa na bunge, wakisema hayakushirikisha wananchi na serikali za majimbo.

#2. Lengo au sababu za Hassan Sheikh kuongeza muda Serikali inasisitiza lengo ni kufanikisha mfumo wa kidemokrasia wa "mtu mmoja kura moja" (universal suffrage) badala ya mfumo wa kizamani wa ukoo. Sababu nyingine ni kuhitimisha mchakato wa kurekebisha katiba uliochelewa, ili kuweka misingi thabiti ya uchaguzi wa moja kwa moja.

3. Kuongeza muda madarakani ili kuleta Demokrasia na UdiktetaNi ngumu kwa wananchi kuamini nia ya kidemokrasia ikiwa kiongozi anatumia muda wa ziada bila kupigiwa kura.Upinzani unaona hatua hii kama ya kiimla na unyakuzi wa madaraka. Wanaharakati wanahofia hatua ya kuongeza muda inazidi kutoa mwanya wa matumizi mabaya ya mamlaka. 

4. Sababu za Viongozi wa Afrika kung'ang'ania madaraka: Tamaa ya kulinda maslahi binafsi, ya kiuchumi na ya kijamii ndani ya tawala. Hofu ya kufunguliwa mashtaka au kushtakiwa kwa makosa waliyoyatenda wakiwa madarakani. Udhaifu wa taasisi huru za kikatiba na mahakama unaotoa mwanya wa kubadili sheria kwa urahisi.

5. Tofauti kati ya swala la Somalia na lile la Burkina Faso (Ibrahim Traore)

Somalia: 

Ni nchi yenye mfumo wa uchaguzi wa kidemokrasia (ingawa ni wa uwakilishi wa koo), ambapo Rais anagombania uhalali wa kikatiba dhidi ya wanasiasa wengine.

Burkina Faso:

 Ni serikali ya kijeshi iliyoingia madarakani kupitia mapinduzi, ambapo kiongozi wa kijeshi (Ibrahim Traore) amesitisha misingi ya kidemokrasia.

6. Hatua ambazo Afrika inapaswa kuchukuaKuimarisha na kuheshimu Katiba za nchi kama sheria mama bila kuzibadili kwa maslahi ya watawala. Umoja wa Afrika (AU) unapaswa kuchukua hatua za kinidhamu mapema na kwa nguvu dhidi ya viongozi wanaoondoa vizingiti vya muda.

Tume huru za uchaguzi zinapaswa kupewa uhuru kamili ili kuondoa mianya ya wanasiasa kuchezea chaguzi.

7. Je, kuna haja ya mataifa ya magharibi kuingilia kati? Mataifa ya magharibi yanaweza kutoa msaada wa kidiplomasia na shinikizo za kiuchumi (kama kuweka vikwazo) kuzuia udikteta.Hata hivyo, uingiliaji wa kijeshi au kisiasa wa moja kwa moja kutoka magharibi unaweza kuleta athari za kiutawala na kupunguza mamlaka ya nchi husika.

Ni vyema zaidi kwa suluhu kuu kutoka ndani ya Afrika kupitia Umoja wa Afrika (AU) na asasi za kieneo. Hata hivyo ni vigumu sana kwa afrika kuifikia Demokrasia ya kweli kwa Sababu mara nyingi watawala wamekuwa wakitumia vyombo vya Dola na rasilimali za nchi zao kukandamiza vuguvugu au harakati za kudai haki, au kuua raia wanaoandama, au kukamatwa kwa Viongozi wa upinzani na kuwaweka kizuizini kama inavyoshuhudiwa sasa Tanzania (Tundu Lissu) na Uganga (Kizza Besigye).

Katika nchi kama Bukina Faso kiongozi wa Kijeshi wa mpito Ibrahim Taore alishatangaza wazi kwa sasa Demokrasia haina nafasi kwenye nchi hiyo. Hivi karibuni kati ya tarehe 28-29 mwezi Mei, 2029, Serikali ya mpito ya Rais Taore ilisimamisha kwa muda miezi mitatu shughuli za Umoja wa jumla wa wanafunzi wa Burkina Faso. Hatua hiyo ilifuatia ukosoaji wa Viongozi wa wanafunzi wa rekodi ya utendaji wa Serikali ya Ibrahim Taore.

Changamoto nyingine kubwa ni tabia ya kulindana kwa watawala walio madarakani na kusaidiana kudhibiti harakati za Asasi za Kiraia na Wanaharakati waopaza sauti kudai uwepo wa misingi ya haki na usawa. Mathalani Rais Ibrahim Taore ni swahiba mkubwa wa Samia Suluhu wa Tanzania ambaye pia ni swahiba mkubwa wa Yoweri Museveni aliyebadisha katiba na kujiongezea muda wa kutawala.


Post a Comment

Previous Post Next Post