Kinyume na taarifa zilizozagaa mitandaoni
na kwenye vyombo vya habari, Serikali ya Kenya imekanusha vikali na kusema haimtambui mfanyabiashara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, na wala hana uhusiano wowote na mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).Serikali ilifuta mchakato wa awali wa Kampuni ya Adani ya India baada ya washirika wake kushtakiwa kwa rushwa nchini Marekani.
#Kanusho la Serikali:
Serikali kupitia Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir imeeleza kuwa kampuni ya mfanyabiashara huyo haikushiriki katika mchakato wa utoaji zabuni wa JKIA na haina uhusiano wowote na mradi huo.
Zabuni za Awali nchini Kenya:
Hakuna rekodi rasmi inayoonesha kuwa mfanyabiashara huyu alishawahi kupewa zabuni yoyote ya serikali nchini Kenya hapo awali, ingawa ni mgeni wa mara kwa mara kwenye ikulu ya Rais Ruto.
Uhusiano na Rais Ruto:
Licha ya uswahiba wake na Rais William Ruto kusambaa mtandaoni na yeye kujinadi kuwa karibu na serikali, ya Ruto, haijathibitishwa rasmi endapo serikali ina ajenda ya Siri katika utoaji wa zabuni hizo au endapo inauweka chini ya jamvi ushiriki wa mfanyabiasha huyo wa Zimbabwe.
Gharama ya Upanuzi:
Kulingana na Waziri wa Hazina John Mbadi, gharama zilizotengwa kwa ajili ya upanuzi huo ni kati ya Ksh. bilioni 154 hadi 155 (sawa na dola bilioni 1.2), na sio Ksh. bilioni 375 kama ilivyokuwa inaripotiwa na vyombo vingine vya habari alisema David Chirchir
Idadi ya Kampuni:
Mkataba huu wa upanuzi wa JKIA unaongozwa na kampuni moja kuu ya serikali ya China, China Communications Construction Company (CCCC), na kampuni tanzu yake ya China Road and Bridge Corporation (CRBC).
Kampuni hizo zinashirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini Kenya (KAA) chini ya Mfuko wa Kitaifa wa Miundombinu.
