Rais Wiliam Ruto Sasa anameelekeza nguvu
kwenye eneo la pwani kama njia ya kujihakikiahia uungwaji mkono endapo eneo la mlima kenya litampatia kisogo.Hii imejidhihirisha wazi kwa mwenendo wake wa kifikia eneo Hilo Kila mara anapotoka kwenye ziara zake za ng,'ambo.
Licha ya kuwepo kwa mipango mingineyo ya uzinduzi wa miradi ya kimaendeleo, mikakati pamoja utekelezaji wa sera za uchumi wa bluu, na udhibiti wa ratiba yake. Eneo hili ni kiungo kikuu na ngome ya kundi la Linda Ground la chama Cha ODM. Uanzishwaji na uzinduzi wa miradi mbalimbali si kwamba unakuja tu Bure ila ni mpango mashuhuri wa Ruto kuhakikisha kwamba kura za eneo la pwani zinasalia chini ya himaya yake.
Miongoni mwa mambo mengine makuu yaliyoratibiwa kumpa kipaumbele ni pamoja na:
*Utekelezaji wa Ajenda ya Uchumi wa Bluu (Blue Economy):
Pwani ina rasilimali kubwa za bahari. Rais mara nyingi hurejea katika eneo hili kushughulikia au kuzindua miradi inayohusiana na usafirishaji, uvuvi, na uwekezaji wa bandari na uchumi wa baharini.
*Mikutano ya Kimataifa na Ukanda wa Pwani:
Mombasa na maeneo ya Pwani huandaa makongamano makubwa ya kimataifa, kama vile mikutano ya mazingira ya baharini na maonyesho ya kitalii.
* Kufungua Miradi ya Maeneo ya Pwani:
Eneo la Pwani lina miradi mingi ya kitaifa, kama vile ujenzi wa barabara za kupita pembezoni mwa mji (Mombasa Southern Bypass), maeneo maalum ya viwanda (SEZ), na usambazaji wa umeme.
Serikali inafanya kazi kuhakikisha miradi hii inakamilika na kufunguliwa kwa umma kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
*Kupunguza Uchovu wa Safari (Jet Lag) na Utulivu Kazini:
Safari za ughaibuni huchukua muda mwingi angani na huambatana na tofauti za saa (jet lag). Kufikia Pwani humpa Rais mazingira tulivu ya angalau kupata mapumziko.
*Kukabili Siasa na hoja za Wananchi akiwa mapumzikoni Ikulu ya Mombasa
