#GACHAGUA BADO ANA HAKI YA KUGOMBEA WADHIFA WOWOTE KISIASA

 Kinyume na baadhi ya watu na Wanasiasa wanavyofikiria, Rigathi Gachagua bado

anaruhusiwa kuwania Urais wa Kenya mwaka 2027. Kulingana na sheria na Katiba ya Kenya, mtu aliyetimuliwa madarakani kwa mashtaka yanayohusiana na maadili na uongozi anaweza kuzuiwa kuwania wadhifa wa umma, lakini kizuizi hiki hakianza kufanya kazi hadi pale mchakato mzima wa rufaa utakapokamilika na kuisha kabisa.

 Aidha Rigathi Gachagua mwenyewe ameweka wazi azma yake ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka wa 2027. Licha ya kuondolewa kwake madarakani (impeachment), sheria na Katiba ya Kenya zinamruhusu kugombea kwa sababu kesi yake ya kisheria bado inaendelea mahakamani.

Kwa maana nyingine ni kwamba swala si kwamba anaruhusiwa kugombea au la ila utategemea na jinsi atakavyojipanga na Wanasiasa wengine wa safu ya mbele ya upinzani kama watamwachia yeye nafasinau yeye ndo atakubali kuwa nyuma ya yule watakayekubaliana kumteua.

Kulingana na wataalam wa sheria, ikiwemo Rais wa Chama cha Wanasheria nchini (LSK) Charles Kanjama, kifungu cha 99(3) cha Katiba ya Kenya kinamwezesha mtu yeyote kuwania wadhifa wa kisiasa hadi pale atakapomaliza njia zote za kisheria za kukata rufaa.

Ukomo wa Kisheria: 

Chini ya Sheria ya Uchaguzi na Katiba ya Kenya, mwanasiasa haruhusiwi kugombea iwapo tu kesi na rufaa zake zote zimetolewa uamuzi na kushindwa (yaani amechoka fursa zote za kisheria).Kuhusu Rufaa: Endapo kesi na rufaa zake zitafika hadi Mahakama ya Rufaa au Mahakama ya Upepo na akashindwa kabisa kesi hiyo, ndipo rasmi ataondolewa sifa ya kugombea Urais au wadhifa mwingine wowote wa umma.

Hukumu ya Mahakama Kuu: 

Mnamo Tarehe 8, mwezi Juni 2026, Mahakama Kuu ilithibitisha kuondolewa kwake madarakani, ingawa ilimlipa fidia ya Shilingi milioni 50 kwa kukiukwa kwa haki yake ya kusikilizwa.

Rufaa Ya Kesi:

 Kutokana na uamuzi huo wa Mahakama Kuu, Gachagua ameamua kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi huo na kusisitiza kuwa bado anastahili kuwania nafasi za umma. 

Msimamo wake wa 2027: 

Gachagua anasisitiza kuwa atakuwa kwenye karatasi ya kura mnamo Agosti 10, 2027, aidha kama mgombea wa muungano wa upinzani au akiungwa mkono na viongozi wengine.

Haki ya Kidemokrasia:

 Ila mradi tu bado anaendelea na mchakato wa rufaa kupinga maamuzi hayo mahakamani, jina lake litabaki halali na anayo haki kamili kikatiba ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi.

Kutokana Mwenendo na taratibu za Kisheria za Kenya kuchukua muda mrefu, Kuna uwezekano wa uchaguzi mkuu wa mwakani kufika kabla ya kukamilika kwa mchakato wa Kisheria unaohusu kesi ya kuondolewa Ofisini kwa Rigathi Gachagua.

Kwa mtazamo kwamba Gachagua hatategemea kushirikiana na chama kingine kuunda muungano, hii Ina maana Kwamba atakuwa debeni kwa tiketi ya chama chake cha DCP.

Toa maoni yako....



Post a Comment

Previous Post Next Post