#EBOLA YAATHIRI USHIRIKIANO WA KENYA NA MATAIFA MENGINE


Serikali ya Israel imeondoa zuio la awali kwa raia wa Kenya kusafiri kwenda nchini humo. Mapema Tarehe 14 Juni 2026, Israel ilikuwa imeziorodhesha kenya miongoni mwa Nchi ambazo raia wake wangepeleka Virusi vya Ebola nchini humo.

Hoja na Dondoo zake:

1. Kwa nini serikali ya Israel iliweka vizuizi vya kusafiri kwa wasafiri kutoka Kenya?

Hofu ya Mlipuko:

 Hatua ya Israel ilitokana na tahadhari ya kiafya ya kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa Ebola kutoka eneo la Afrika ya Kati.

Uamuzi wa Mamlaka ya Uhamiaji:

 Mamlaka ya Usimamizi wa Mipaka ya Israel ilitoa agizo la dharura linalozuia mashirika ya ndege kuruhusu wasafiri wa kigeni wanaotoka au waliotembelea mataifa kadhaa ya Afrika ndani ya siku 21 zilizopita kuingia nchini humo ikiwemo Kenya.

 Hata hivyo, agizo hili halikuwaathiri raia au wakaazi wa Israel.

2. Kwa nini hatua hiyo ilichukuliwa na Israel ili hali Kenya haina kisa chochote cha Ebola? 

Hatua ya Tahadhari ya Kikanda:

 Ingawa Kenya haikuwa na kisa hata kimoja, Israel iliiorodhesha pamoja na nchi nyingine zenye maambukizi (kama DRC na Uganda) ili kujikinga na uwezekano wa mlipuko kuvuka mipaka. 

Mwitikio wa Kenya:

 Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ililalamika vikali ikieleza kuwa hatua hiyo haikuwa ya haki kwa vile hakuna kisa chochote Cha Ebola kilichoripitiwa Nchini Kenya.

Hii ni baada ya Serikali kutoa taarifa inayoonyesha  kupima zaidi ya sampuli 80,000 na zote kuonekana hazina Ebola.

Ubatilishwaji wa Marufuku:

 Kufuatia malalamiko hayo ya kidiplomasia, Wizara ya Afya ya Israel iliondoa Kenya kwenye orodha ya nchi zenye vizuizi vya Ebola. Hata hivyo licha ya Kenya na Rwanda kuondolewa kwenye orodha ya Nchi ambazo raia wake walipigwa marufuku kuingia Israel, Bado chanzo Cha hatua hiyo ya Serikali ya Israel kinasalia kuwa uamuzi wa Kenya Kutanguliza Maslahi ya watu wa nje kuliko raia wake kwa kufanya maamuzi ya awali ya kukubali kuwaleta wagonjwa wa Ebola kutoka nje bila yenyewe kuwa na visa vya maambukizi.

3. Je, mgogoro wa kituo cha Ebola kinachojengwa Laikipia ulichangia uamuzi wa Israel?

 Kulikuwa na mkanganyiko:

 Kituo chenye mgogoro Cha karantini ya Ebola ya Laikipia ni miongoni mwa Sababu za maamuzi ya  Israel na mataifa mengine kuitazama Kenya kama eneo lenye hatari ya mlipuko na kuchukua tahadhari hasa baada ya kuzuka kwa maandamano, migomo, vurugu na vifo.

Ukweli wa Mradi wa Laikipia:

 Kituo hicho kilichozua taharuki na maandamano ni mpango wa ushirikiano kati ya Kenya na Marekani (ulioidhinishwa na wizara ya afya) kujenga kituo cha kutolea huduma kwa Wamarekani wenye maambukizi au walio kwenye hatari ya maambukizi ya Ebola.

Hatua hii awali ilizua mvutano na pingamizi kutoka kwa wananchi, wanasiasa na vyama vya madaktari kufuatia hofu za kiafya.

Mpango huo hata hivyo ulisimamishwa na mahakama ya kenya.

Post a Comment

Previous Post Next Post