Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, anaruka.viunzi na kusingizia Kwamba Kikosi maalum cha Nairobi Metropolitan Police Unit (NMPU) kitakachoanzishwa kwa mkataba wa ushirikiano kati ya serikali kuu na ya Kaunti ya Nairobi kitasaidia kudhibiti wahuni na magenge ya uhalifu jijini Nairobi.kwa sababu zifuatazo:
Mbinu za Kina na Ushirikiano:
Kikosi hiki kina mfumo maalum wa kiintelijensia na uratibu unaolenga kipekee mazingira magumu ya kiutawala na uhalifu ndani ya jiji la Nairobi.
Kudhibiti Wanasiasa na Wafadhili:
kikosi hiki kitatumika kutokomeza mbinu za wanasiasa wanaofadhili makundi ya wahuni (kama ilivyoshuhudiwa katika matukio ya All Saints Cathedral).
Ulinzi wa Biashara na Raia:
Lengo kubwa la kikosi hiki ambacho muundo wake unatokana na ushirikiano wa kimataifa kama wa Polisi wa New York na London, ni kulinda mali na miundombinu dhidi ya uhalifu unaoathiri uchumi wa jiji.
Kwa mujibu wa Waziri Murkomen, Serikali kupitia wizara husika imewekeza katika kubadilisha mbinu za kiusalama ili kukabiliana na matukio ya utumiaji nguvu na uharibifu unaotokana na shinikizo na ufadhili wa Wanasiasa.
Waziri Murkomen alitoa maelezo haya mnamo Juni 14, 2026. alipokuwa akihutubia waumini katika Kanisa la AIC Plainsview jijini Nairobi, kufuatia ghasia zilizofanywa na wahuni waliovamia kongamano lililokuwa likiendelea katika Kanisa Kuu la All Saints Anglican Cathedral .Alisisitiza kuwa kikosi hicho maalum na mbinu za kiintelijensia zitatumika kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wahusika.
Mikakati:
Udhibiti wa wanasiasa wanaounga mkono serikali:
Ili serikali ikabiliane na wanasiasa hawa iwe wanatoka upande wa upinzani au serikali iliyopo madarakani Waziri Murkomen msimamo mkali kwamba sheria itachukua mkondo wake bila woga au upendeleo. Jambo ambalo hata hivo hadi sasa limeshindikana.
Uchunguzi wa Kijasusi:
Kitengo cha DCI kinafuatilia kwa karibu kamera za usalama (CCTV), video, na data ya mawasiliano ili kubaini nani anawafadhili, jinsi wanavyolipwa, na kuwashtaki kwa kosa la kufadhili uhalifu.
Kutochagua Upande (Non-Partisan enforcement):
Kukataa kuwalinda wanasiasa hata kama wana msimamo wa kuiunga mkono serikali; hatua kama ya kuwakamata viongozi na wafadhili wa magenge iwapo ushahidi utapatikana.
Kuvunjwa kwa mitandao: wa Wahuni:
Kukata mizizi ya ufadhili wa kiuchumi, kuwashtaki wahalifu wenyewe, na kutumia sheria za NCIC.Kutoa onyo rasmi: Kutoa maagizo ya wazi kutoka kwa Idara ya Polisi chini ya Inspekta Jeneral.
Kwanini Maelezo ya Murkomeni ninHekaya za Abunuasi:
*Kuna kesi Mahakamani:
Kuna kesi Mahakamani inayopinga ushirikiano wa Serikali kuu na Kaunti ya Nairobi ambayo haijaamiliwa. Kwa kutegemeana na mwenendo wa kesi hiyo, ushirikiano huo unaweza kuvunjwa au kuondolewa kwa baadhi ya vigezo na masharti ya mkataba.
*Kukithiri kwa Visa vya Magenge ya Wahuni:
Swala la kuwepo kwa magenge na vikundi vya wahuni havijaanza leo wala.jana. waziri mwenye dhamana ya Usalama wa ndani wa Nchi anaposema kwamba licha ya kuwa Vyombo vyote vya Dola anategemea kuanzishwa Kwa kikosi Cha Naira Metropolitan polisi kudhibiti wahuni ni unafiki wa wazi. Je kikosi hicho kisipokuwepo?
*Magenge ya Wahuni yapo kote nchini na sio Nairobi pekee:
Je, kikosi hicho Cha Nairobi metropolitan polisi Cha Nairobi kitafanya kazi Nchi nzima? Bado maeneo mengine ya Nchi yanahitaji kudhibiti.
*Je Kwanini hatuoni mikutano ya Rais Ruto au wandani wake ikivurugwa?
Swali hili tumeliuliza mara nyingi, kwamba wahuni wanaonekana zaidi kwenye mikutano ya wapinzani. Lakini mikutano mingine yote ya viongozi wa Serikali au Viongozi waliopo kwenye mlengo wa serikali mikutano yao haivurugwi?
*Magenge ya Wahuni yanafadhiliwa na Wanasiasa wa Kambi ya Serikali:
Tatizo kubwa ni kwamba vikundi na magenge ya Wahuni wanaosumbua maeneo mengi Nchini wanafadhiliwa na Wanasiasa wenye mlengo wa kuunga mkono Serikali. Matokeo yake, Viongozi wa Serikali nao wanasimama majukwaani na kuwanyooshea vidole wapinzani kwa dhana ya unafiki huku wakijua wazi kinachoendelea.
Hii maana yake ni kwamba Kipchumba Murkomen, DIG Douglas Kanja, na Mohammed Amin wote wanajua kinachoendelea. Huu yumkini ni Mradi wa Serikali iliyopo madarakani kuelekea uchaguzi ujao wa mwaka 2027.