Hivi majuzi Rais wa Tanzania Samia Suluhu ameteua tume nyingine ya uchunguzi inayoelezewa kuwa ya Kijinai baada ya Ile ya Jaji Othman
Chande iliyotoa taarifa yake rasmi 23 Aprili 2026, ikiwiwa ni mwendelezo wa mlolongo wa Tume zinazotarajiwa kuundwa na Rais huyo.Tume hii iliundwa rasmi tarehe 18 Mei 2026, mahususi kwa ajili ya kufanya Uchunguzi wa Kijinai wa matukio ya vurugu na ghasia yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Tume hiyo ipo chini ya uenyekiti wa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Shabani Ally Lila, akisaidiwa na Makamishna watatu ambao ni majaji wastaafu wa Mahakama Kuu: Gad Mjemmas, Awadh Bawazir, na AishieliS umari.
Hadidu za Rejea za Tume:
Kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi (Sura ya 32), hadidu za rejea kuu za tume hii ni
I) Kuchunguza Vurugu za Uchaguzi:
Kufanya uchunguzi wa kina wa kijinai kuhusu matukio yote ya ghasia yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
ii) Kuwabaini Waandaaji na Wafadhili:
Kuwatafuta na kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika kupanga, kuratibu na kufadhili vitendo hivyo vya uhalifu.
iii) Kufuatilia Vifo na Watu Waliopotea:
Kuchunguza kwa undani taarifa za vifo, madai ya miili ya watu kutopatikana, na watu wanaodaiwa kutekwa na wasiojulikana.
iv) Kushughulikia Waathirika:
Kufuatilia matukio ya watu waliopata madhara (ikiwemo nje ya maeneo ya vurugu) ili kuhakikisha haki inapatikana na kuwezesha uwajibikaji.
Tume ya Jaji Chande:
Tume ya Jaji Othman Chande: Ilikuwa ni Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani (iliyokabidhi ripoti yake mnamo Aprili 23, 2026). Kazi yao ilikuwa ni kukusanya maoni, kuchunguza vyanzo, ukubwa wa tatizo, athari, na kutoa mapendekezo mapana ya kisera na kitaasisi ya nini kilisababisha vurugu hizo.
Tume ya Jaji Shabani Lila (Sasa):
Hii ni Tume ya Uchunguzi wa Kijinai. Tofauti na ile ya kwanza, tume hii ina nguvu za kiupelelezi (kama polisi au vyombo vya dola) ili kutafuta ushahidi thabiti wa kisheria utakaowawezesha kuwatambua, kuwakamata, na kuwafungulia mashitaka watu binafsi au makundi yaliyovunja sheria.
Je, Watanzania Watarajie Nini?
Watanzania wanatakiwa kutarajia ripoti itakayofichua ukweli thabiti wa kiuhalifu na mwenendo mzima wa Matukio:
Ikiwa ni pamoja na:
I) Wafadhili wa vurugu hizo na machafuko: hasa kama ni Serikali ya Tanzania, Ni wapinzani wa Serikali, Ni mashirika au Asasi za Kiraia, Ni Wageni kutoka nje,n.k
ii) Malengo au Nia ya Wafadhili
iii) Mipango hiyo ilianza lini na ilihusishanwakina nani?
Iv)Ni Misitu gani? Ya maeneo yapi ya Nchi pamoja na Majengo yalipotolewa mafunzo ya watu walioshiriki uhalifu na Vurugu hizo? Kwanini hawakujulikana?
v) Wapi ilipo Miili ya watu wasiopatikana hadi leo? Wapi yalipo makaburi ya halaiki? Ni Lengo la kufichwa kwa miili ya wahanga wa vurugu/ machafuko hayo.
Vi) Je Watu waliohusika kutekeleza Vurugu hizo walikuea watanzania au raia kutoka nje? Na endapo walitoka nje, iweke Vyombo vya ulinzi na usalama wa Nchi havikuwabaini?
Vii? Ni Kweli Kuna watu waliotolewa hospitalini wakiwa Bado kufariki na kupelekwa kusikojulikana? Na akina nani?
Viii) Ni Kweli Kuna watu ambao hawakuwa kwenye maandamano waliofuatwa majumbani mwao na kuuawa?
Ix) Mchango na Nafasi ya mitandao ya kijamii.
X) Ushiriki wa Serikali na Vyombo vya Dola.
xi) Agizo/Amri ya kutotoka nje, je ilizingatia Sheria?
xii) Nani aliyezima mitandao? Kwamagizo la nani?
xiii) Nani aliyezima Umeme? Kwa agizo la Nani?
xiv) Ushiriki wa Tume ya Uchaguzi ya Tanzania:
*Je, uchaguzi ulifanyika? Katika mazingira gani?
*Tume ya Uchaguzi iliwezaje kufanikisha uchaguzi katika Mazingira yale, hususan ukusanyaji, majumuisho na kutangazwa kwa matokeo katika mazingira Giza nchi nzima na ukosefu wa mitandao?
Endapo hoja au maswali haya hayatajibiwamna Uchunguzi wa tume hiyo basi watanzania wajue Bado wanatwanga maji kwenye kinu.
