#JAMES ORENGO NOW RISKS BEING IMPEACHED

 #Gavana wa Siaya James Orengo yumo kwenye hatari ya kuondolewa kwenye nafasi yake. Hii ni kutokana na

msimamo  wake wa Kisiasa unaopinga Ushirikiano wa chama Cha ODM na kile Cha UDA Cha Serikali ya Kenya kwanza, ikiwa ni pamoja na hatua yake ya kukimega chama hicho na kuunda kundi pinzani la Linda Mwananchi pamoja na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna.

Aidha hatua ya kiongozi huyu kutoa lugha ya kashfa kwa Gavana wa Homa Bay, Gladys Wanga, iliyoashiria kuwa udhalilishaji wa kijinsia imekoleza moto wa hasira za wapinzani wake na kuelekea kupanda kwa joto la Kisiasa ndani ya Kaunti ya Siaya ambayo pia ni Ngome ya Oburu Oginga, kinara wa sasa wa ODM.

 Aidha, Madiwani wa Baraza la Siaya wekusanya sahihi zenye lengo la kumng'atua kutoka Ofisini. Taarifa za karibuni zinaonyesha huenda ikawa ya sahihi hizo ikatimia kumwezesha hoja ya kutokuwa na imani na Gavana huyo.

#Katika hatua nyingine, Timu nzima ya usalama ya Gavana wa Siaya James Orengo, pamoja na walinzi wake wa kibinafsi na wale waliokuwa wakilinda makazi yake jijini Nairobi, iliondolewa ghafla usiku wa tarehe 19 Mei 2026 bila taarifa yoyote ya awali au kupatiwa mabadala.

Chanzo/Sababu;

Ingawa polisi hawakutoa sababu rasmi mara moja, kuondolewa kwa walinzi hao kulijiri baada ya malalamiko makali na utata wa kisiasa kufuatia matamshi ya kibabe na utata ambayo Gavana Orengo anadaiwa kutoa dhidi ya Gavana wa Homa Bay, Gladys Wanga.

Hatua Zilizochukuliwa na Orengo:

Katika hali ambapo usalama wa afisa wa serikali unaondolewa kinyume cha utaratibu, gavana Orengo  ameandika barua rasmi ya malalamiko kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IG) na Waziri wa Usalama wa Ndani.Kudai maelezo ya kimaandishi na ya kina kuhusu kutababu za kuondolewa kwa walinzi hao na Kutaka kurejeshwa mara moja kwa maafisa hao kwa kuwa ulinzi sio upendeleo bali ni haki yao kikatiba.

#Hata hivyo imekuwa ni desturi kwa Serikali ya Kenya kuondoa walinzi wa viongozi wanaoasi au kuwa Wapinzani na wakosoaji  wake.

 Usiku wa kuamkia Tarehe 25 November 2025, Walinzi wa Gavana wa kaunti ya Trans-nzoia, David Natembeya waliondolewa bila taarifa kwa kile kilichotafsiriwa kama hatua yake ya kuwa mpinzani na mkosiaji wa Serikali.

Toa maoni yako.....


Post a Comment

Previous Post Next Post