Jina la Dennis Itumbi ni miongoni mwa majina yaliyogonga vichwa vya habari kwenye mchakato mzima wa kutatua Mgomo wa shirikisho
la wamiliki wa Vyombo vya usafirishaji nchini Kenya. Hii ilitokana na kutafutwa na vongozi hao wa vyama vya usafirishaji ili kufanikisha kikao na Viongozi wa Serikali hasa pale jitihada zao zilipokwama.Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amemtuhumu yeye na msaidizi mwingine wa Rais Farouk Kibet, kuendesha serikali. Madai haya yanatokana na ukweli kwamba Itumbi ameonekana akiongoza mikutano ya serikali na Viongozi wa usafirishaji badala ya mawaziri pindi Rais William Ruto akiwa nje ya nchi.
Hata hivyo, madai haya ya Gachagua yanaonekana kama mbinu za kisiasa kuliko ukweli thabiti. Licha ya kuwepo kwa Ombwe la kukosa kiongozi aliyeweza kufikiwa kwa haraka kuwasikiliza wawakilishi hawa wa vyombo vya usafirishaji, uhalisia ni kwamba Itumbi ndiye aliyeweza kufikiwa kwa haraka baada ya mawaziri husika kuonekana kuruka viunzi.
Ukweli ni kwamba mawaziri husika David Chirchir (Barabara naUsafirishaji) na Mwenzake Opiyo Wandayi (Nishati na Mafuta) waliona siku kuwa ndefu baada kuwekwa kiti moto maswali ambayo hawakuwa na majibu. Walipatikana kwa kuchelewa na hata baada ya kufika kwenye kikao kile walionekana kunyeshewa mvua na kukosa majawabu.
Kimsingi hawakuwa na cha kusema baada ya kutoa taarifa ya kuwepo makubaliano iliyopingwa na Viongozi wa vyama vya usafirishaji. kwa mtazamo wetu tunadhani Gachagua anakolezea kuvutia kwake.
#1. Dennis Itumbi ni nani?
Dennis Itumbi ni Mkuu wa Miradi Maalum na Uchumi Bunifu katika Ofisi ya Rais William Ruto.
Mkakati wa Kidijitali:
Ni mtaalamu wa mikakati ya kidijitali na mwanahabari wa zamani. Alijipatia umaarufu mkubwa kupitia uandishi wa blogu na kuratibu kampeni za mitandao ya kijamii zilizomwingiza madarakani Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta na baadaye Rais William Ruto.
Nafasi Yake Serikalini:
Mwaka 2024, Rais Ruto alimteua rasmi kuwa Mkuu wa Miradi Maalum na Uchumi Bunifu katika Ofisi ya Rais. Katika nafasi hii, jukumu lake rasmi linahusisha kuratibu ubunifu wa maudhui ya kidijitali na kusimamia miradi maalum ya rais.
#2. Tuhuma zaGachagua:
Kwanini Gachagua anamshutumu Itumbi kuongoza Serikali ya Ruto?
Mikutano ya Serikali (Viral Meeting):
Gachagua alidai kuwa pale Rais William Ruto anapokuwa nje ya nchi, wasaidizi wake, hasa Itumbi, ndio huongoza shughuli za serikali badala ya maafisa wakuu kama vile mawaziri. Shutuma hizi ziliibuka baada ya mkutano mkuu uliohusisha mawaziri na viongozi wa sekta ya uchukuzi kusambaa mtandaoni wakati wa mgomo, ambapo Itumbi alionekana mstari wa mbele kuchukua jukumu kubwa.
Ushawishi wa Ndani:
Gachagua alidai katika mahojiano kuwa Rais Ruto husikiliza na kuongozwa zaidi na Itumbi pamoja na Farouk Kibet kuliko hata mawaziri au washauri wengine rasmi wa serikali.
#3. Ukweli wa Madai ya Gachagua:
Uchambuzi wa wanasiasa wengi na wachambuzi wa siasa za Kenya unaonesha kuwa madai ya Gachagua yana uzito mdogo wa kiutawala, badala yake yana uzito mkubwa wa kisiasa:
#Ukweli wa Kisiasa:
Ni wazi kuwa Dennis Itumbi ana ushawishi mkubwa katika uendeshaji wa ajenda za Rais Ruto. Hata hivyo, Itumbi mwenyewe amejitokeza na kufafanua kwamba hafanyi kazi kwa matakwa yake, bali anatekeleza majukumu rasmi aliyopewa na ofisi ya Rais. Madai ya Gachagua yalipamba moto hasa baada ya yeye kung'atuliwa mamlakani na kusimama nje ya utawala.
#4. Uzito wa Kisheria na Kiutawala:
Ukweli Kikatiba/Kisheria:
utendaji wa serikali hauwezi kuongozwa na msaidizi wa kibinafsi au mwanablogu peke yake. Mawaziri ndio wanaofanya maamuzi na kuwajibika kisheria. Hivyo, kudai Itumbi ndiye anayeendesha serikali nzima ni mtazamo unaotumiwa kisiasa ili kuonyesha kuwa viongozi walioteuliwa hawana sauti.
Ugomvi wa Binafsi:
Itumbi aliwahi kufichua kwenye mahojiano kuwa kabla ya mzozo huu wote, Gachagua alitaka amwandike kwenye mitandao ya kijamii kama 'mfalme' au kiongozi mkuu wa Mlima Kenya. Itumbi alipokataa, walifikia hatua ya kukabiliana ana kwa ana. Hivyo, shutuma hizi pia zinatafsiriwa kuwa matokeo ya chuki ya binafsi.
Hitimisho:
Wakati Itumbi akiwa na nguvu na ushawishi wa karibu na Rais kupitia asasi za miradi maalumu, kauli za Gachagua kwamba Itumbi ndiye anayeamua kila kitu serikalini zinachukuliwa zaidi kama maneno ya kisiasa kutoka kwa kiongozi anayetafuta kuhoji utawala uliopo baada ya kuondolewa madarakani.
Toa maoni yako....
