#MIGOS OGAMBA RESIGNS? Is it possible in Kenya?

 Kutokana na mkasa wa moto katika Shule ya Utumishi (Utumishi Girls Academy), Waziri wa Elimu Julius

Migos Ogamba pamoja na Waziri wa Ndani Kipchumba Murkomen walitakiwa kujiuzuru. 

Katika kipindi hiki ambacho Shule za Bweni zinaonekana kuwa kimbio la wazazi kwa Usalama na Elimu Bora kwa watoto huku Shule nyingi za kutwa zikiwa kwenye hatari za kufungwa, Waziri Migosi Ogamba amedinda kujiuzuru kutoka na mkasa wa moto Shule ya wasichana Utumishi Girls.

Sababu za Msingi za kumtaka Waziri wa Elimu Kujiuzuru:

Nani walizotoa Madai hayo:

1. Viongozi wa Kisiasa na Mashirika na Asasi za Elimu, Wanaharakati wamemtaka Waziri Migos Ogamba Kujiuzuru

Chama cha Demokrasia kwa Wananchi (DCP): Chama hiki, kiongozwa na aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua, kilitoa wito wa kumshinikiza Waziri Ogamba na Waziri wa Ndani Kipchumba Murkomen kuwajibika na kujiuzuru.

Kundi la Elimu Bora na Tume ya Haki za Kibinadamu nchini (KHRC): Makundi haya ya kiraia yalianzisha shinikizo hili kama sehemu ya utetezi wa usalama wa wanafunzi. 

2. Sababu za Kushinikiza Kujiuzuru

Viongozi na wanaharakati hao walitoa sababu zifuatazo:

Kushindwa Kusimamia Usalama wa Wanafunzi:

Wamedai kuwa viongozi hao walishindwa kuhakikisha shule za bweni zina viwango stahiki vya usalama na utayari wa kukabiliana na majanga.

Uzembe wa Taasisi za Elimu:

Walisisitiza kuwa Wizara ilishindwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa miundombinu kama njia ya kinga badala ya kusubiri majanga yatokee. 

Kujirudia kwa Matukio ya Moto Mashuleni

Tukio la mkasa wa Moto Utumishi Girls sio la kwanza nchini kenya na kila mara yametolewa maelezo ya kufanyika utuchunguzi usiokuwa na tija kwa wazazi na walezi wanaopoteza watoto wao.

3. Je, Waziri Ogamba Atajiuzuru?

Waziri Migos Ogamba hajatangaza kujiuzuru. Badala yake, serikali kupitia wizara husika imesisitiza kuwa maafisa wa upelelezi (DCI) na wataalamu wanafanya uchunguzi kubaini chanzo cha mkasa huo, na imewataka Wakenya kuepuka minong'ono hadi uchunguzi ukamilike. 

4. Sakata la Uagizaji Mafuta la Waziri Opiyo Wandayi

Mwezi Aprili, Waziri wa Nishati na Petroli, Opiyo Wandayi, alikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa Wabunge, Asasi za kiraia na Wanaharakati kumtaka ajiuzuru kufuatia kashfa ya uagizaji wa mafuta duni yenye thamani ya mabilioni ya shilingi nje ya utaratibu wa serikali. Licha ya viongozi wengine katika wizara yake kujiuzuru, Waziri Wandayi alikataa vikali kujiuzuru na badala yake alitetea nafasi yake akisema hakuhusika na kuidhinisha uingizaji wa mafuta hayo. 

5. Idadi ya Mawaziri Walionusurika au Kutakiwa Kujiuzuru kwenye Serikali ya Ruto:

Kwenye serikali ya Rais William Ruto, shinikizo kwa mawaziri kujiuzuru limekuwa likijitokeza mara kwa mara wakati wa matukio ya kitaifa yenye utata.

Waziri Opiyo Wandayi: 

Alikuwa waziri wa kwanza kwenye baraza hili jipya (kufuatia mabadiliko ya serikali ya mseto) kushinikizwa vikali kujiuzuru.

Waziri Julius Migos Ogamba:

 Anakuwa waziri wa pili kutakiwa na viongozi kujiuzuru kufuatia misiba ya moto katika shule ya Utumishi Girls,

Hata hivyo, hakuna taarifa zinazoonyesha kuwa Waziri Ogamba amekubali kujiuzuru, kwani amesisitiza kusubiri uchunguzi na kuendelea na kazi yake.

Lakini Je Kwanini inakuwa vigumu kwa mawaziri wa Serikali ya Ruto kujiuzuru pale yanapotokea Matukio ya uzembe.

Uteuzi wa Kisiasa na Mikataba: 

Mawaziri wengi ni wanasiasa au washirika wa karibu ambao walichaguliwa kulipa fadhila za kisiasa na kuwakilisha jamii zao. Kujiuzuru kunaweza kuchukuliwa kama usaliti dhidi ya mrengo wao wa kisiasa.

Hofu ya Kupoteza Kinga na Ushawishi:

 Nyadhifa za uwaziri huwapa ushawishi mkubwa wa kiuchumi na kijamii. Kuondoka ofisini mara nyingi kunamaanisha kupoteza kinga ya kisiasa inayoweza kuwaweka wazi kwa uchunguzi wa matumizi mabaya ya ofisi.

Mwenendo wa Rais na Mfumo:

 Katika historia ya siasa za Kenya, utamaduni wa mawaziri kujiuzuru kwa hiari ni nadra sana. Badala yake, wengi hungoja hatua ya Rais kuwafuta kazi. Mara nyingi Rais huwatetea au kuwahamishia wizara nyingine badala ya kuwashinikiza waondoke, kama ilivyoshuhudiwa katika mabadiliko ya awali.

Kutokubali Makosa:

 Mara nyingi viongozi hawa hukataa kukubali lawama moja kwa moja, wakiamini matatizo yanayojitokeza yanasababishwa na changamoto pana za kiuchumi, ukosefu wa fedha, au siasa. 

Hata hivyo, katika mazingira ya siasa za Kenya, mawaziri waliotajwa wameendelea kushikilia nyadhifa zao huku wakijitetea na kusubiri taratibu za kisheria au uchunguzi ukamilike badala ya kuchukua hatua ya kuachia ngazi.



Post a Comment

Previous Post Next Post