#TANZIA: KUHUSIANA NA MKASA WA MOTO UTUMISHI GIRLS

 Tumepokea kwa masikitiko makubwa Janga la msiba wa moto ulioteketeza bweni la Shule ya wasichana ya

Utumishi Girls eneo la Gilgil kaunti ya Nakuru, ambapo wanafunzi 16 wamefariki Dunia kwa kuteketea kwa moto na wengine 79 kujeruhiwa.

Tunapenda kuwafariji familia za wafiwa, ndugu jamaa, marafiki kwa familia zilizofikwa na umauti na wale waliojeruhiwa katika mkasa huo.

Wakati hayo yakijiri ni matarajio yetu kwamba Vyombo vya Serikali vitabaini mambo muhimu kuhusiana na mkasa huo ikiwa ni pamoja:

I) Endapo Shule ilikuwa na walinzi na kama walikuwepo shuleni wakati kisa hicho.

ii) Kwanini Walinzi hawakutoa taarifa ya mapema kuhusiana na tukio hiloiii) Kujua chanzo Cha moto endapo ni hitihalafu au ulisababishwa na mtu.

iv) Miundombinu ya bweni lililoungua kama ilikidhi viwango kwa mujibu wa sera ya Elimu kuhusiana na majengo ya shule. Milango na madirisha ya dharula.

v) Mpangilio wa vitanda navifaa vinginevyo ndani ya bweni ikiwa ni pamoja na nafasi kati vitanda.

vi) Uwajibikaji wa Mkuu wa Shule na walimu walezi na WA vitengo husika.

Kupatikana kwa taarifa hii ni muhimu kwa wadau wa elimu ili kuepuka kisa kama kujirudia tena kwa Shule hiyo na zinginezo kote nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post