#KUPATA NAFASI YA KAZI KENYA LAZIMA UVAMIE JUKWAA LA RAIS

Mtu aliyevamia jukwaa la Rais William Ruto alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara eneo la Ganze Kilifi mkoa wa Pwani Mei 24, 2026, amelipwa fadhila kwa kupewa nafasi ya kazi kwenye Shirika la Mamlaka ya Bandari Nchini Kenya.

Taarifa zilizovuja kwenye mitandao ya kijamii Jumatatu mei 25, 2026, zinazonyesha mtu huyu ambaye jina lake halijabainishwa anasadikiwa kupewa nafasi ya ajira kwa kitendo chake Cha kuvamia jukwaa la Rais na kusababisha taharuki.

Endapo taarifa hizi zitathibitishwa kuwa za Kweli hiki litakuwa ni kitendo Cha ajabu, Cha kusikitisha na kukatisha tamaa.
Wakati taifa likiwa kwenye taharuki ya kuongezeka kwa visa vya watu kuibuka na kuvamia jukwaa la Rais Ruto akiwa kwenye mikutano ya Kisiasa, kitendo Cha mtu aliyefanya tukio kama hilo kupewa kipaumbele Cha ajira ni taswira mbaya.

Ikumbukwe kwamba tukio hilo limefuatiwa na hatua nyingine nyingi ikiwemo:
1. Serikali kuchukua hatua ya kuwabadilisha maafisa wa Usalama waliohudumu kwenye kikosi cha Ulinzi kwenye msafara wa Rais ambapo William Sawe amechukua nafasi ya Noah Maiyo Maiyo ambaye amehamishiwa kwingine.

2. Kuimarisha ulinzi wa Rais maradufu ya jinsi iliyokuwa awali.

3. Kuongeza idadi ya maafisa wa vikosi vya Jeshi la Polisi wanaomlinda Rais.
4. Kuanzisha uchunguzi kuhusu sababu na mazingira yanayosababisha kujitokeza kwa visa hivyo.

Mtazamo/Matarajio kwa Jamii:
1. Picha inayoweza kujitokeza kwa Wananchi ni kwamba kitendo kile ni sawa na si uvunjaji wa sheria.

2. Kwa wakenya wengi wenye masaibu ya kukosa ajira ni lazima mtu atafute nafasi ya kuonana na Rais au kwa kumvamia jukwaani ndo anahatike.

3. Ili kupata ajira nchini Kenya ni lazima ufanye kituko fulani Cha kufanya mtu aonekane tofauti na wengine.

4. Ni ishara kwamba mtu huyo si mhalifu ila ni shujaa na mfano wa kupigwa.
5. Upendeleo dhidi ya wengine ambao huenda wapo waliokuwa na sifa zaidi yake Waliachwa au kupuuzwa.
5. Kuna maswali muhimu miongoni mwa wakenya endapo Mamlaka ya Bandari ilikuwa na nafasi wazi? Kuna nafasi za ajira zilizokuwa zimetangazaa? 
6. Hoja ya kutolewa nafasi za ajira kwa kujuana, bila kuwa na anayekujia hujapata kazi Kenya.
7. Kasi ya tukio lenyewe ni jambo la kushtua. Tukio limefanyika Mei 24,2026 na Mei 25, 2026 mtu huyu amepata kazi. Je alitumia maombi lini? Alisailiwa na kukaguliwa lini? Ni maswali nyeti.

Mtandao huu hatukuweza kuthibitisha habari hii kwa haraka japo tunafuatilia mamlaka za bandari kuthibitisha taarifa hizi lakini kwa kuzingatia Kwamba lisemwalo lipo, na kama halipo nasi laja.

Toa maoni yako...

Post a Comment

Previous Post Next Post