#JOHN MBADI ATOKWA KIJASHO CHEMBAMBA KUTETEA BAJETI YA SERIKALI YA 2026/27

 Waziri wa fedha wa Kenya John Mbadi  yuko kwenye bustani ya Jeevanjee Garden mjini Nairobi leo Mei 26, 2026, akipokea

maoni na kujibu maswali ya Wananchi kuhusu mapendekezo ya mapato na matumizi kwenye mswada wa fedha wa mwaka 2026/27.

Hatua hii ni utekelezaji wa hitaji la kikatiba linalohitaji kushirikishwa kwa Wananchi kabla ya mswada wa fedha kuidhinishwa na kupitishwa na Bunge.

Hata hivyo hakuna ratiba maalumu iliyotolewa kwa Umma kuhusiana na maeneo mengine yanayotarajiwa kufanyika mikutano ya aina hii kote nchini ili kuwapatia Wananchi fursa ya kutoa maoni kwenye mswada wa fedha wa mwaka 2026/27.

Hatua hiyo ni muhimu ili kukidhi uiano wa uchangiaji wa maoni kwa wananchi kote nchini. Ni matumaini ya wakenya kwamba mijada hiyo haitaishia Mijini pekee.


Post a Comment

Previous Post Next Post