Mwenyekiti wa tume ya Uiano na Utangamano ya Kenya NCIC, Dr Kepha Omae ameogopa kumchukulia hatua za kinidhamu Katibu Mkuu wa chama
cha UDA, kwa kauli na matamshi yake ya hivi karibuni yaliyochochea Chuki na utengano kati ya jamii ya Mlima kenya na Jamii zingine za kenya.Inasadikiwa Kwamba baada ya kuapishwa majuzi tarehe 20, Mei 2026, Dr Kepha anahofia kushusha rungu moja kwa moja kwa kiongozi wa chama kinachounda Serikali ya Rais William Ruto. Hata hivyo taarifa za kina zinaeleza kuwa Sheria inaitaka tume kupokea malalamiko, kufanya uchunguzi wa kina, kukusanya ushahidi, na kumwita mhusika ili kujieleza kabla ya kufungua mashtaka au kutoa adhabu rasmi. Hadi kufikia sasa hakuna malalamiko rasmi yaliyowasilishwa na mtu yeyote mbele ya tume hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari mei 24, 2026, Dr Kepha aliishia kulaani na kutoa onyo kwa matamshi ya Hassan Omar ambayo kimsingi yalivuka mipaka ya Kisiasa na kulenga kabila au Jamii ya wakiyu, na kumlenga zaidi Rais msitaafu Uhuru kenyatta na familia yake, kwa kuwatukana na kuwadhalilisha kama "Vikaragosii"
Matamshi ya Katibu Mkuu wa Chama cha UDA, Hassan Omar, yaliyozua utata yalimlenga Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na Jamii ya Mlimani (Kikuyu). Kauli hizo zilitolewa wakati wa mkutano wa kisiasa huko Mombasa mnamo Mei 2026, ambapo aliomba msamaha mnamo Mei 24, 2026. Kufuatia hilo, Tume ya Uwiano na Utangamano (NCIC) ilianzisha uchunguzi rasmi badala ya kutoa onyo la haraka.
Tarehe ya Tukio:
Matamshi hayo yalitolewa na Hassan Omar Tarehe 21 Mei 2026, wakati wa hafla ya utoaji wa hati miliki za mashamba iliyofanyika Kaunti ya Mombasa, hafla iliyohudhuriwa na Rais William Ruto.
Kuomba Msamaha:
Hassan Omar alitoa taarifa rasmi ya kuomba msamaha Jumapili, Mei 24, 2026. Katika taarifa hiyo, alieleza kuwa maoni yake yalichukuliwa nje ya muktadha na hakukusudia kuudhi au kulenga jamii yoyote.
Hatua za Chama Cha UDA:
Hadi sasa, hakuna hatua zozote za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi ya Hassan Omar na chama chake cha UDA kutokana na matamshi hayo. Badala yake, wanasiasa wengi wa upande wa serikali hawakukosoa kauli hizo hadharani, jambo lililozidisha hasira kutoka kwa viongozi na wananchi wa Mlima Kenya.
Uchunguzi wa Tume ya NCIC:
Uchunguzi wa NCIC unajumuisha kutathmini muktadha mzima wa matamshi yake, athari za uchochezi zilizojitokeza kwenye jamii, na uchunguzi wa video na sauti ili kubaini kama alikiuka sheria za utangamano. Pia, tume inachunguza kama kuna mitandao au viongozi wengine wanaochochea uhasama wa kijamii.
Hatua ya Tume ya NCIC:
Hadi sasa, Tume ya NCIC imelaani na kutoa Onyo. Tume imewataka wanasiasa kuacha lugha zinazoweza kuleta mgawanyiko wa kikabila, jambo linaloashiria msimamo wao wa kulaani aina hiyo ya siasa bila kumtaja Hassan Omar pekee.
Ujumbe wa Hassan Omar Ulisheheni nini?
Hassan Omar alidai kuwa baadhi ya viongozi wa Mlima Kenya na wafanyabiashara waliofungamana na Uhuru wanajaribu kutumia nguvu na mabavu dhidi ya serikali iliyopo madarakani. Pia alihoji hatua ya matatu kususa kufanya kazi chini ya utawala wa Rais Ruto ilhali walivumilia changamoto kama hizo za kiuchumi wakati wa utawala wa Uhuru.
Maana ya Ujumbe wa Hassan Omar:
Hassan Omar alimaanisha kwamba kuna njama za kisiasa nyuma ya maandamano yanayohusiana na gharama za maisha. Alihimiza wananchi wenye kutoridhishwa kusubiri hadi mwaka wa uchaguzi wa 2027 ili kutumia haki yao ya kidemokrasia badala ya kuvuruga utawala wa sasa.
HITIMISHO:
Katika kipindi hiki ambapo taifa linaelekea kwenye maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, ni vema time ya NCIC kushika hatamu, isitokee Kuwepo baadhi ya viongozi wa vyama au Serikali wanaoweza kuligawa taifa kwa kauli au lugha za Uchochezi kisha wakakimbia kuomba msamaha baada ya kuwasha moto wa ghasia na machafuko.
Kila kiongozi awajibike kwa matendo na kauli zake.
