Mgomo wa wasafirishaji Bado Unaendelea. Hii ni kwa Sababu ya kutofikiwa kwa makubaliano yoyote kati Serikali na wasafirishaji. Mgomo wa vyombo vya uchukuzi nchini Kenya uliosababishwa na ongezeko la bei ya mafuta umekwamisha
shughuli zote za kijamii na kiuchumi nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu wanne (4) kote nchini. Serikali imekataa kupunguza bei hizo na inasisitiza kuwa bei ni za soko la kimataifa.Athari za Mgomo wa Uchukuzi:
Mgomo huo uliohusisha matatu, bodaboda, teksi, na malori uliacha maelfu ya wananchi wakiwa wamekwama katika vituo mbalimbali. Watu wengi walilazimika kutembea kwa miguu ili kufika kazini, huku shule na Masoko zikisalia fungwa katika baadhi ya maeneo, na shughuli za kibiashara zilisimama huku waandamanaji wakifunga barabara na kuwasha mioto.
Idadi ya Waliofariki:
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Mambo ya ndani Kipchumba Murkomeni,Watu wanne walithibitishwa kufariki nchini kote kutokana na makabiliano hayo ya vurugu za maandamano na mgomo. Watu wengine zaidi ya 30 walijeruhiwa, na wengine 348 walikamatwa na polisi kufuatia machafuko hayo.
Msimamo wa Serikali Kuhusu Bei ya Mafuta:
Serikali haijaridhia kupunguza bei hizo, ikiongozwa na kawi na Mafuta , Opiyo Wandayi,Waziri wa fedha John Mbadi pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen. Serikali imeeleza kuwa bei hizo mpya (ambapo petroli inauzwa kwa shilingi 214.25 na dizeli shilingi 242.92 kwa lita jijini Nairobi) zitasalia hadi kipindi kijacho kitakachotangazwa.
Serikali inatetea hili kwa kusema linatokana na mgogoro wa Mashariki ya Kati na gharama za soko la dunia, ingawa inatumia ruzuku kidogo kudhibiti kupanda zaidi kwa dizeli.
Kuhusu Kupanda kwa Bei ya Mafuta Nchini Kenya:
Hadi kufikia sasa Serikali ya Kenya imeshindwa kufafanua kwa Umma kwanini viwango vya bei ya mafuta Kenya viko juu kuliko mataifa jirani.
Kuhusu madai ya bei kuwa maradufu (mara mbili zaidi) kuliko nchi jirani kama Uganda na Tanzania, Shirika la Kitaifa la Wafanyabiashara na Viwanda Kenya (KNCCI) limetoa taarifa rasmi inayokiri kwamba Kenya inasalia kuwa miongoni mwa masoko ya mafuta yanayotoza gharama za juu zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Hata hivyo, ingawa si "maradufu" (mara mbili), tofauti hizo hutokea kutokana na viwango tofauti vya kodi za ndani, ada za maeneo ya bandari, na utaratibu wa uagizaji wa Mafuta kutoka nje.
