Je, Ni Kweli Kwamba Wanaume Husinzia Mara tu Baada ya Tendo la Ndoa?


 Swali: Je, ni kweli wanaume hulala haraka baada ya kufanya ngono? Hali ikoje kwa wanawake?

Jibu:

Ni kweli kwamba wanaume mara nyingi hulala haraka zaidi baada ya tendo la ndoa kuliko wanawake. Hii inasababishwa na mambo ya kibiolojia na kimwili kama:

Hormoni za Prolactin: 

Baada ya mwanamume kufika kileleni (orgasm), mwili hutoa kiasi kikubwa cha hormoni ya prolactin, ambayo inasababisha uchovu mkubwa na kusinzia.

Uchovu wa Kimwili: 

Wanaume mara nyingi hutumia nguvu nyingi kimwili wakati wa tendo, jambo linalofanya misuli kuhitaji kupumzika. 

Hali ikoje kwa wanawake?

Wanawake pia huhisi kusinzia kutokana na homoni ya oxytocin inayotolewa, lakini mara nyingi wanawake wanahitaji kubembelezwa (cuddle) au kuongea baada ya tendo, jambo linaloweza kuwafanya wasilale haraka.

Tafiti zinaonyesha kuwa kama wote wawili watafika kileleni, tofauti ya kusinzia hupungua, na wote wanaweza kusinzia kwa wakati mmoja.

Kusinzia kwa mwanamume si ishara ya kutokujali, bali ni majibu ya kawaida ya kibiolojia. 


Post a Comment

Previous Post Next Post