
Akizungumza leo mbele ya Kamati ya Bunge inayohusika
ma maswala ya Mafuta' Energy and Petroleum Committee ' Waziri Wandayi ameimbia kamati hiyo kwamba akiwa Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Kawi na Mafuta, hakujua na hakujulishwa chochote kuhusiana mchakato mzima wa uagizaji Mafuta ghafi kutoka nje.Wandayi ameitupia lawama kamati inayohusika na ukaguzi wa viwango na ubora wa Mafuta kwamba ndo hasa iliyobeba jukumu hilo. Kamati hiyo ya watu 29 ndio iliyokuwa ikiomgozwa na Viongozi wakuu wa idara na vitengo vya Serikali vinavyohusika na uagizaji wa Mafuta waliofunguliwa mashataka ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya takriban Pesa za Kenya Ksh Bilioni 2.9 .
Maafisa walioshtakiwa na kisha kujiuzuru ni pamoja na: Mohammed Liban, Joe Sang, Daniel Kiptoo na Joseph Wafula.
Wandayi pia ameileza kamati hiyo kwamba uchunguzi unaoendelea kuhusiana na Sakata hilo utadhihilisha kutohusika kwake.