#Magenge ya Wahuni ' Je, Ni Mradi wa Serikali?

 # Wimbi la Uhalifu Nchini: Siasa, Lawama na Hofu ya Wananchi

Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya maeneo nchini kenya yameshuhudia ongezeko la visa vya wahuni na majambaz wakiharibi Mali za watu, kupiga na kujeruhi na kusababisha hofu miongoni mwa jamii. Matukio yaliyorekodiwa katika maeneo ya Kikuyu, Kitale na Kisumu kati ya Tar 9 -11 Aprili 2026, yameacha maswali mengi kuhusu hali ya usalama na uwajibikaji wa vyombo husika.

#Hali ya Usalama  Imekuwa Tete.

Matukio haya yamekuja kwa kasi na kwa mtindo unaofanana. Tukio la hivi karibuni zaidi ni lile la tarehe 11 Aprili 2026 huko Kikuyu, ambapo vurugu na uharibifu wa mali uliripotiwa, hasa kwenye eneo la Barabara ya 'Southern by Pass' huku madai yakielekezwa kwa wanasiasa kwa kurushiaana mpira, kuhusu ufadhili wa machafuko hayo.

Aidha, tukio la kusikitisha la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Seneta wa Vihiga, Godfrey Osotsi, limeongeza wasiwasi kuhusu usalama wa hata viongozi wa umma.

# Siasa za Lawama:  Nani Anasema Ukweli?

Katika hali inayoonekana kuwa ya kulaumiana, viongozi wa kisiasa kutoka pande zote wamekuwa wakirushiana lawama kuhusu chanzo cha machafuko hayo.

Kwa upande wa upinzani, viongozi kama Babu Owino, Edwin Sifuna na Kalonzo Musyoka na Wanasiasa wenzao wamenukuliwa wakilaumu serikali kwa kushindwa kudhibiti usalama na hata kudai kuwa kuna mkono wa serikali katika baadhi ya visa hivi. Babu Owino na Edwin Sifuna wamemnyooshea kidole Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani, Raymond Omollo, wakimtaka ajiuzuru kwa kile wanachodai ni uzembe au kushindwa kutekeleza majukumu yake.

#Kauli Tata Kutoka Serikalini

Hata hivyo, kauli iliyozua mjadala mkali zaidi ni ile ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Kipchumba Murkomen. Waziri huyo licha ya kumtetea  Katibu wake katika Wizara hiyo, Raymond Omollo, alidai hivi majuzi  kwamba magenge ya wahuni na majambazi yanayohusika kuharibu mali za watu na kuvuruga amani yanapangwa na kufadhiliwa na wanasiasa wa upinzani wanaovaa vema suti zao na kuingia maofisini mwao kupanga uhalifu, kisha baadaye hujitokeza hadharani kuilaumu serikali na kuwataka Viongozi husika Serikalini wajiuzuru.

Kauli hii imeibua maswali mazito kutoka kwa wananchi na wachambuzi wa siasa:

* Ikiwa serikali ina taarifa za wanasiasa wanaofadhili uhalifu, kwa nini hawakamatwi na kufikishwa mahakamani?

* Kwa nini mikutano ya hadhara ya Wanasiasa wa upinzani ndiyo inalengwa zaidi na vurugu hizi?

* Kwa nini wahuni hawaonekani kuvuruga mikutano ya Rais au ya viongozi wanaomuunga mkono?

*Ni kwa nini Serikali haichukui hatua za haraka kunusuru hali? Mfano katika Tukio la hivi majuzi pale Kikuyu, Wahuni na Majambazi walijinafasi muda mrefu na  mchana kweupe bila Vyombo vya Dola (Polisi) kufika eneo la tukio huku wakipora na kuharibu mali za watu 

*Je, Wanasiasa wa upinzani wanaweza kupanga mipango au kufadhili wahuni kuvuruga mikutano yao wenyewe?

Maswali haya yanaacha pengo kubwa la uaminifu kati ya wananchi na vyombo vya dola.

#Kauli Zinazokinzana?

Waziri wa mambo ya ndani Kipchumba Murkomeni ameanza kuwa na rekodi ya Kauli na matamko yanayokinzana,. Itakumbukwa kwamba Waziri Murkomeni amewahi kunukuliwa akisema kwamba mabomu ya kutoa machozi yanayotumika kuvuruga mikutano ya wapinzani yanamilikiwa na raia na kwamba alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Mohammed Amin kuchunguza swala hilo. 

Hata hivyo hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kwa Umma endapo Kuna raia yeyote aliyekamatwa na bomu la aina hiyo. Awamu  hii Waziri Murkomeni amekuka na kauli kwamba Viongozi wa Upinzani ndio wanaofadhili magenge ya Wahuni ili kujivurugia mikutano yao wenyewe. Aidha amerudia kauli ileile kwamba amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Upelelezi wa siasa ya Jinai kufanya uchunguzi. 

Itoshe kusema kwamba katika jamii iliyostaarabika, kiongozi anapotoa kauli juu ya jambo lenye maslahi kwa Umma au lonaloathiri jamii kwamba lichunguzwe, ni vema pia majibu ya uchunguzi ule yatolewe kwa Umma na kwa uwazi.

Je, kauli hizi zisizo na tija zinaweza kuleta suluhu au zinachochea mkanganyiko zaidi? Ni matarajio yetu kwamba kwa kuwa serikali inamiliki Vyombo vya Dola na uwezo wote wa kuweza kudhibiti matukio hayo bila shaka tungeliwaona Wahusika wakiwa wamefikishwa mbele ya Sheria bila kujali vyeo au umaarufu wa mtu.

# Nafasi ya Viongozi Kuhakikisha Usalama wa Raia na Mali zao 

Wakati siasa zikichukua nafasi kubwa katika mjadala huu, ukweli usiopingika ni kuwa wananchi wa kawaida ndio wanaoathirika zaidi. Biashara zinaharibiwa, maisha yanahatarishwa, na hali ya hofu inaongezeka. Chukulia mfano tukio la tar 11 Aprili, 2026, huko Kikuyu hasa Ile Barabara ya 'Southern by Pass' 

*Kuna magari na wasafiri walizuiliwa kuendelea na safari zao

*Magari mengine yalitobolewa tajiri zao

*Biashara za watu zilifungwa 

*Mali kuharibiwa

*Athari za kiuchumi na kijamii, sasa nani anayeweza kuwalipa fidia Wananchi wale?

Inasadikiwa kwamba Kimani ichungwah  ndiye aliyepanga na kufadhili wahuni katika tukio Lile hasa kwa lengo la kumzuia Gachagua kufanya mkutano wa Siasa kwenye eneo linaloaminika kuwa ngome yake, na baadaye alijitokeza na kulaani tukio alilolipanga mwenyewe.

Mzizi wa fitina unaonekana kuwa kulipiza kisasi kwa kauli za Gachagua alizozitoa wiki Jana kwenye mazishi ya David Njuguna kiaraho huko Ol kalao.

Na kama hiyo haitoshi taarifa zinasema kwamba Kimani ichungwah amenukuliwa kwa mara nyingine akisema Kwamba kiongozi wa DCP, Rigathi Gachagua ndiye aliyehusika kupanga vurugu zile na anapaswa kuchunguzwa na kwamba Wahusika walitoka nje ya eneo la Kikuyu.

Ni matarajio yetu kwamba ni jukumu la viongozi wote serikalini na upinzani kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya siasa za lawama. Kauli zao zina nguvu, na zinaweza ama kutuliza hali au kuchochea zaidi taharuki.

# Hitimisho

Wimbi hili la uhalifu linahitaji majibu ya haraka, ya wazi na ya haki. Wananchi wanahitaji kuona hatua zikichukuliwa, si kusikia lawama zikielekezwa kila upande.

Swali kuu linabaki: Je, taifa linaelekea wapi ikiwa usalama wa raia na Mali zao unageuzwa kuwa uwanja wa siasa?

Bila uwajibikaji wa kweli na hatua madhubuti, hofu ya wananchi itaendelea kukua na imani yao kwa viongozi wao kupungua. Hii ndo maana uchambuzi wetu unatufanya kufikiria kwamba licha kuwepo uhuru wa kikatiba wa uhuru wa maoni, kutangamana na kukusanyika katika midhara ya kisiasa, huenda ni mradi wa serikali kuiminya demokrasia  na kuzima sauti za wapinzani kuelekea uchagizi Mkuu ujao wa mwaka 2027.

Post a Comment

Previous Post Next Post