#SERIKALI YA RAIS RUTO SASA YATOA MAKUCHA

Kwa mara ya kwanza tangu kuingia madarakani Serikali ya Rais William Ruto imejizatiti kuonyesha

makali yake kwenye ufisadi na ubadhili unaondelea kwenye Wizara, Idara na Vitengo vya Mafuta. 

Hatua hii imedhihirika baada ya kukamatwa Tar 2, Aprili 2026, kwa Maafisa wakuu wa Idara na Vitengo vinavyohusika na uagizaji wa Mafuta ghafi kutoka ng'ambo. Miongoni mwa Walikamatwa ni Daniel Kiptoo ambaye alishikilia wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Udhibiti wa Nishati, Mohammed Liban ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Idara ya Serikali inayoshughulikia Mafuta na Joe Sang ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kenya Pipeline.

Maafisa hao ambao pia walijihuzuru nyazifa zao Tar 4, April 2026,  kufuatia kukamatwa kwao wanatuhumiwa kuhusika na kashfa ya uingizaji wa mafuta usiofuata sheria wenye thamani ya Shilingi bilioni Bil 4.8. Aidha wanatuhumiwa kuchakachua data za mafuta ili kuunda uhaba bandia na kuagiza mafuta duni na ghali zaidi.

Lakini hoja kubwa hapa ni endapo serikali ya Rais Ruto Hatimaye itakuwa na dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi katika idara na vitengo vya Serikali.

Kufika Mahakamani:

Watatu hao walipangiwa kufika mahakamani Jumanne, Aprili 7, 2026, kufuatia kuachiliwa kwa dhamana ya polisi huku wakisubiria kufika mahakamani.

Ni matarajio ya wakenya kwamba kesi hii itachukua mkondo thabiti wa haki bila mikingamo au mizengwe inayoweza kuwatakatisha.

Siasa na Nishati:

Ingawa maafisa hawa wa ngazi ya juu walijiuzulu, Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi bado yuko ofisini, jambo ambalo limeibua maswali kuhusu kuwepo  uhusiano au ushawishi wa kisiasa au  mgongano wa kimasilahi katika Sakata hili. Kuendelea kuwepo Ofisi kwa Waziri mwenye dhamana ya Nishati, Opiyo Wandayi , kunatoa taswira ya uwezekano wa Maafisa hawa kutumiwa kama "Kondoo wa kafara'  kulinda wanasiasa wa juu.

Haki ya Mahakama:

Wakenya wana matumaini mseto kuhusu ikiwa kesi hiyo itakuwa na haki au itapangwa kama mchezo wa karat ili kisha kuwaachilia huru washukiwa, ikizingatiwa kuwa Joe Sang aliwahi kushinda kesi kama hiyo hapo awali.

Kwa sasa' macho na masikio ya wakenya yameelekezwa kwenye muhimili wa mahakama kwa yatakayojiri Hatimaye.


Post a Comment

Previous Post Next Post