Rais Paul Biya amekuwa kiongozi wa Cameroon, aliyeingia madarakani Novemba 6, 1982 hadi leo, hii inamfanya kuwa mmoja wa viongozi waliokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi duniani, akiwa na umri wa miaka 93 (kufikia Aprili 2026) , katika kipindi hicho Rais Biya ameitawala Cameroon kwa mkono wa chuma.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Al jazeera Paul Biya amemteua mwanawe Franck Emmanuel Biya, kuwa Makamu wa Rais kwa Amri ya Rais ya Tar 4,2026.
Wadhifa wa Makamu wa Rais
Sheria mpya ya Cameroon inasema Makamu wa Rais atachukua kiti cha Urais moja kwa moja iwapo Rais Paul Biya atakufa, kujiuzulu, au kutokuwa na uwezo wa kuhudumu.
- Mabadiliko ya Katiba: Uteuzi huu umekuja siku chache baada ya bunge la Cameroon kuridhia mabadiliko ya katiba ambayo yalirudisha nafasi ya Makamu wa Rais kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1972.
- Kusudi: Watazamaji wa kisiasa wanaona hatua hii kama mkakati wa Paul Biya (mwenye umri wa miaka 93) wa kuandaa mrithi wa kiti cha urais (succession plan) kutokana na umri wake mkubwa.
1. kumrithisha Madaraka (Dynastic Succession): Kuhakikisha nguvu inabaki katika familia na kulinda utajiri na urithi wa Biya.
2. Uaminifu: Katika umri wa miaka 93, Biya amemweka karibu mtu anayemwamini zaidi ili kuzuia mapinduzi ya kijeshi au kisiasa.
3. Kuzuia Migogoro: Kujenga njia ya kisheria ya mrithi kuzuia mapambano ya madaraka ndani ya chama tawala.
Mtazamo katika Siasa za Afrika
Hatua hii inaonyesha mwenendo wa viongozi kushikilia madaraka (life presidency) kama wanavyofanya Marais wengine wa Afrika kama vile
#Yoweri Museveni (Uganda): Mipango ya kurithisha madaraka kwa mwanawe.
#Paul Kagame (Rwanda): Kukandamiza upinzani na kuimarisha utawala.
#Ibrahim Traoré (Burkina Faso): ambaye ameupinga waziwazi mifumo Demokrasia wa kimagharini na kuimaarisha utawala wa kiimla.
Athari za Muda Mfupi na Mrefu
Muda Mfupi:
Maandamano, misukosuko, ghasia,kuongezeka kwa ukandamizaji, mauaji, na kutokuaminiana kijeshi.
Muda Mrefu:
Uchumi kudorora, taasisi za kiserikali kudhoofika, na hatari ya machafuko kifo cha kiongozi kitakapotokea.
Watu wa Afrika Wafanye Nini?
Uraia Hai: Kushiriki kikamilifu katika mashirika ya kiraia kutaka uwajibikaji.
Kuunganisha Upinzani: Upinzani uliogawanyika unawapa viongozi hawa nguvu.
Aktivism ya Kidijitali: Kutumia mitandao ya kijamii kufichua ukandamizaji na kuhamasisha vijana.
