
Taarifa zilizopatikana awali zinasema kikosi hicho kimekwenda huko kwa ajili ya mafunzo na utafiti wa kijeshi. Hata hivyo Kuna utititi wa maswali kuhusiana na ziara hiyo. Kubwa zaidi ni endapo nchi yenye misukosuko na ukosefu wa kiusalama,inayochechemea kujiimarisha au kujijenga kisiasa , kijamii, au kiuchumi inaweza kuwa uwanja wa mafunzo au utafiti wowote kutoka kwenye nchi iliyotulia kijeshi au kiusalama.
Rais mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alikwenda Burkina Faso katikati ya mwezi Aprili 2025. Ziara yake ilihitimishwa jijini Ouagadougou tarehe 17 Aprili 2025.
Lengo la Ziara ya Kikwete hata hivo halikufahamika zaidi ya hoja moja tu, kwamba alibena ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kumkabidhi Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Captain Ibrahim Traoré.
Katika hili ni vema kujitafakari kwamba ni ujumbe gani huu muhimu ambao ungeyarajiwa kutoka Kwa Rais aliyeshinda uchagizi wenye vurugu na utata, kwenda kwa Rais mwingine wa kiimla aliyetwaa madaraka kwa mapinduzi na kisha kuizima demokrasia na kuikalia nchi kimabavu?
Taarifa zilizopatikana baadaye hata hivyo zilisema ziara Ile ililenga kuimarisha uhusiano wa kibalozi, ushirikiano wa kiulinzi, na kubadilishana uzoefu kati ya nchi hizo mbili. Jiulize ni uzoefu upi ambao Tanzania inaweza kupata kutoka Bukina Faso? Hapo ndipo mkakati huu wa siri ulipoanza na mtaalamu huyu wa mikakati, Rais msitaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Ni baada ya Ziara ile ya Kikweye ambapo kikosi Cha jeshi kutoka Tanzania kimepelekwa Bukina Faso. Kulingana na ushirikiano huo, vikosi vya Tanzania vinaenda Burkina Faso kuisaidia nchi hiyo, hasa katika maeneo ya mafunzo na kubadilishana uzoefu wa kiusalama. Hilo huenda linafanyika chini ya kivuli Cha sehemu ya mikakati ya nchi za Afrika kutafuta "suluhisho la Kiafrika kwa matatizo ya Afrika". Lakini ndani ya hoja hizi yapo mambo yaliyofichika.
Nani anatoa mafunzo? Ushirikiano huo unaonekana kuwa wa pande mbili ambapo wataalamu wa Tanzania wanatoa mafunzo na uzoefu katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na utawala, ulinzi ,kilimo na madini, huku kubwa zaidi likiwa ushirikiano wa kijeshi.
Sasa nani anamsaidia mwenzake? Huu ni ushirikiano wa kimkakati. Lakini ni ukweli usiofichika kwamba Tanzania inakwenda kumsaidia Taore kuitawala Bukina Faso. Haya mengine ni kufunika kombe.
Sehemu ya habari hii imetolewa kwenye channel ya Africa perspective miongoni mwa vyanzo vingine.