
Juzi Dunia imeshuhudia Shirika la Serikali ya Marekani linalohusika na utafiti wa anga za juu na safari za ndege (NASA) likituma chombo kingine katika anga za juu baada ya miaka 50. Chombo hiki kwa jina Orion kinatarajiwa kuuzunguka Mwezi mara kadhaa kabla ya kurejea tena duniani.
NASA inasimamia ' National Aeronautics and Space Administration' NASA. NASA ilianza rasmi kazi zake mnamo Oktoba 1, 1958. Hata hivyo, chombo chake cha kwanza cha utafiti kilichofanikiwa (satellite) kilikuwa Explorer 1, kilichorushwa tarehe 31 Januari 1958 (kabla ya kuanzishwa rasmi kwa ofisi hiyo, lakini chini ya usimamizi wa kijeshi uliohamishiwa NASA baadaye). Safari ya kwanza ya mwanaanga wa Marekani (Alan Shepard) ilikuwa Mei 5, 1961.
NASA imetuma vyombo vingi anga za juu, lakini mafanikio ya kutua kwa binadamu (Apollo Missions) yalikuwa mara 6 kati ya mwaka 1969 na 1972.
Safari hizo ni Apollo 11, 12, 14, 15, 16, na 17.
Kumbuka: Apollo 13 ililazimika kurudi bila kutua mwezini baada ya ajali, na kulikuwa na safari nyingine za anga za juu za utafiti (orbital/uncrewed) kabla na baada ya kipindi hicho.
NASA inaendelea na mpango wa Artemis, ambapo misheni ya Artemis II ilirushwa Aprili 3-4, 2026, ikiwa ni safari ya kwanza ya wanaanga kuzunguka mwezi baada ya miaka 50. Mafanikio ya chombo hiki Cha Orion kilichoondoka kwenda anga za juu na wanajimu wanne (4) japo yakisalia kuwa siri ya NASA na Serikali ya Marekani ni hatua inayosubiriwa kwa hamu.