MAREKANI NA ISRAEL ZASHINDWA VITA DHIDI YA IRAN

kulingana na taarifa zilizothibitishwa   Ijumaa Tar 3 April, 2026 na Shirika la Habari la Uingereza (BBC) na pia Shirika la Habari la Ujerumani

(DW), ndege ya kivita ya Marekani aina ya F-15E Strike Eagle ilidunguliwa katikati mwa anga ya Iran. 

Aidha, wanajeshinwa Iran wamo mbioni kuwasaka marubani wawili ambao wanaaminika kunusurika kutoka kwenye ndege hiyo, na mamlaka nchini Iran zimetangaza zawadi nono kwa yeyote atakayewakamata marubani hao wakiwa hai.

Ndege  iliyodunguliwa na Iran ni F-15E Strike Eagle. Aidha, ripoti zinaonyesha kuwa ndege nyingine ya kivita ya Marekani aina ya A-10 Thunderbolt II ilipata ajali aukushambuliwa katika eneo la Ghuba ya Uajemi wakati wa operesheni za uokoaji.

 Wakati hayo yakijiri Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amemfuta kazi Afisa  Mkuu wa majeshi wa nchi hiyo, Randy George pamoja na maafisa wengine waandamizi wawili.

Taarifa zinasema kumekuwepo shinikizo la uongozi, huku ripoti nyingine zikimhusisha Jenerali wa jeshi la nchi kavu kuondolewa ghafla.

Inaaminika kwamba Sababu za kutimuliwa  wakuu wa jeshi ni pamoja na mwenendo wa Matukio katika Iran. Hasa kudumhuliwa kwa ndege za Kisiasa kabisa za Marekani  juu ya anga ya Iran. 

Kuangushwa kwa ndege hizo za kivita (F-15E na A-10) na kushindwa


kwa operesheni za uokoaji (ikiwa ni pamoja na helikopta kupigwa risasi wakati ikijaribu kumwokoa rubani) kumeibua maswali mazito kuhusu usalama na uwezo wa kijeshi wa Marekani dhidi ya Iran.

 Tukio hili la kudunguliwa kwa ndege ya kivita ya Marekani kwenye anga ya iran ni pigo kubwa kwa utawala wa Trump hasa baada kutamba mara kadhaa kwamba majeshi ya Marekani kwa kushirikiana na Yale ya Israel yameyadhoofisha kabisha majeshi ya Iran.

Post a Comment

Previous Post Next Post