Mbunge wa viti Maalimu County ya Murang'a' amewasha
moto mitandaoni baada ya kula kiapo kuvua nguo na ikibidi hata chupi yake ilimradi tu kama itafaa kuwashawishi watu wa Murang'a' kuhudhuria kwenye Ziara ya Rais William Ruto iliyopangwa kuanza Ijumaa hii tar 24 Aprili 2026.Mitandaoni hivi sasa kumezagaa taarifa ya kiapo Cha Mbunge huyu akisema, na hapa tunamnukuu, "Mimi hata suruali ya ndani nitawatolea Bora tu msikose kutolewa kupokea Rais Ruto hapa Murang'a on Friday" bila shaka hakuna vazi linalojulikana kama suruali ya ndani, ila kwa maana nyingine Sabina alimaanisha chupi.
Japo wanaohudhuria mikutano ya siasa huwa ni wake kwa kwa waume, haijajulikana bayana kwamba ni kundi lipi hasa analolilenga Mbunge huyu.
Sabina Chege ni mwanasiasa mashuhuri nchini Kenya, kwa sasa ni Mbunge Aliyeteuliwa (Nominated MP) na aliwahi kuwa Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Murang'a (2013–2022). Kabla ya kuingia siasani, alikuwa mtangazaji wa redio na mwigizaji mashuhuri.
Kauli za Kisiasa za Hivi Karibuni na Msimamo:
Uungaji Mkono kwa Ruto:
Baada ya kumuunga mkono Raila Odinga mwaka wa 2022, alihama na kuahidi kufanya kazi na serikali ya Rais William Ruto (Kenya Kwanza) mnamo Mei 2023.
Kupinga Maandamano:
Hivi karibuni, amepinga maandamano ya vijana (Gen Z), akisema kuna njia bora za kushughulikia masuala, na kuwataka vijana kusubiri uchaguzi wa 2027.
Kupinga 'Zoning':
Amekosoa mikakati ya 'zoning' (kugawa maeneo) hasa na chama cha ODM, akiiita mbinu ya ubinafsi.
Kuhusu madai ya kuvua nguo:
Kulingana na ripoti za habari za hivi punde, madai kwamba Sabina Chege ameahidi kuvua nguo ili kuvutia watu kwenye mkutano wa Rais Ruto huko Murang'a hayajathibitika. Jukwaa hili hata hivo halijashuhudia ripoti yake binafsi , video, au habari zozote za kuaminika zinazothibitisha kutoka kwa Sabina Chege.
Kwa vile siku yenyewe haijafika hili ni swala la muda
