Watanzania na Dunia nzima kwa jumla Wana hamasa na kiu
ya kutaka kujua kilichomo kwenye ripoti ya Tume ya Jaji Chande ambayo kwa taarifa zilizopo inatarajiwa kukabidhiwa Samia Suluhu Ijumaa ya tar 23 Aprili 2026 jijini Dar es salaam.Kulingana na taarifa za hivi karibuni (Aprili 2026), Tume Huru ya Uchunguzi ya Matukio ya Vurugu za Uchaguzi inayoongozwa na Jaji mstaafu Mohamed Chande Othman imepokea ushahidi kutoka kwa wananchi 63,603, ikionyesha kuwepo kwa ushirikiano na matumaini kutoka kwa baadhi ya wadau.
Hata hivyo, ripoti ya Tume hiyo imeghubikwa hisia mchanganyiko na ukosefu wa imani kwa baadhi ya wananchi na wanasiasa dhidi ya tume hiyo na vyombo vya uchaguzi kwa ujumla vinatokana na sababu zifuatazo:
Sababu za Kutokuwa na Imani
Muda Kuongezwa:
Tume iliomba nyongeza ya mara pili ya siku 21, jambo ambalo liliibua hofu kuwa kunaweza kuwa na utaratibu wa kuchelewesha au kubadilisha matokeo ya uchunguzi.
Hofu ya Kuingiliwa:
Pamoja na Jaji Chande kusisitiza kuwa tume yake haingiliwi, wasiwasi wa kihistoria wa tume zinazoundwa na Rais kutokuwa huru kikamilifu bado upo kwa baadhi ya wananchi.
Mazingira ya Uchaguzi Mkuu (Oktoba 29, 2025
Tume hiyo ilikuwa ikichuguza vurugu zilizotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ambao ulikumbwa na Vurugu na machafuko makubwa jambo linalofanya hitimisho lolote kuonekana lenye utata.
Kuna hisia za kuwepo walakini kwenye ripoti hiyo endapo itatoa majibu ya wazi Kwa baadhi ya maswali, kwa mfano endapo:
* Je, itaeleza kama kweli upipaji kura uliofanyika ?ulifanyika vipi katikati ya vurugu? Au endapo uchaguzi huo ulikuwa huru?
*Kama itafafanua mchakato mzima wa Uchaguzi, tume ya uchaguzi nchini humo ilifikiaje ushindi kwa Samia Suluhu, au Tume hiyo ya uchaguzi ilifanikiwa vipi kuhesabu kura kwa kipindi kifupi bila mwanga Wala uwezo wa mtandao? Au endapo Samia Suluhu alishinda kiharali?
*Je, Itaepuka kutaja uwepo/ uwezekano wa ufadhili kwa baadhi ya watu au makundi ya watu walionunuliwa kufanya vurugu.
*Je, Itamsafisha na kutomhusisha Samia Sulumu kwenye machafuko hayo.
*Je, itaepuka Kutowahusisha Wala kuwataja viongozi waandamizi wa Serikali ya Samia.
* Je, itakwepa au Kutoeleza au kuweka bayana ilipopelekwa miili ya watu waliouawa kwenye machafuko hayo.
*Je, ripoti hiyo itaeleza Asili ya Wahusika kama walitoka nje ya nchini kama ilivyonukuliwa kauli ya Samia Suluhu
* Kuna tetesi kutoka ndani ya Serikali na chama Cha CCM zinazodokeza uwezekano wa ripoti hiyo kumwelekezea lawama kiongozi wa upinzani Tundu Lissu ambaye yuko kizuizini.
*Kuna uwezekano mkubwa wa ripoti ya Jaji Chande kuelekeza chanzo Cha vurugu kuwa Uchochezi wa Tundu Lissu, hii ni muhimu ili kuharalisha ushahidi wa kumtia hatiani.
*Ushiriki wa vyama vya upinzani: Kuna uwezekano mkubwa wa ripoti hiyo kivitumia lawama vya upinzani hasa Chadema ili kusafisha serikali ya Samia Suluhu.
Je, Wajumbe ni Sababu?
Mtazamo Chanya: Wafuasi wa tume hiyo wanawataja wajumbe, wakiongozwa na Jaji Chande, kama watu "wabobevu" na wenye weledi wa hali ya juu, wakiamini heshima ya Jaji Chande itasaidia kupata ukweli. Hata hivo wanahofiwa kutegemea upande wa Serikali.
Mtazamo Hasi: Wanaopinga Time hiyo wanaona kuwa tatizo si wajumbe mmoja mmoja pekee, bali ni mfumo wa uteuzi wa tume hiyo (kuteuliwa na Rais ambaye ni mtuhumiwa namba Moja), jambo linaloweza kuwafanya wasiwe huru kikamilifu katika kutoa ripoti inayomwajibisha mwajiri wao.
Hitimisho:
Imani kwa tume ya Jaji Chande imegawanyika; wapo wanaoiamini tume hiyo, hasa wakereketwa wa chama Tawala CCM, kutokana na weledi wa wajumbe wake, na wapo wanaotilia shaka matokeo yake kutokana na mazingira ya kisiasa nchini Tanzania na ukubwa wa vurugu zilizotokea. Hili ni kundi kubwa la wapinzani na Wananchi wa kawaida.
Macho na masikio sasa ni kusubiri siku yenyewe.
