#KIWINGU CHA MAANDAMANO CHAYEYUKA

Maandamano yaliyokuwa yamepanga kufanyika leo Tar 21 April 2026 kushinikiza punguzo la bei ya mafuta yamefeli. Hivi karibuni pamekuwepo mashinikizo kutoka kwa Wanasiasa wa upinzani na wanaharakati yanayohamasisha kifanyika maandamano siku ya Jumanne yenye lengo la kushinikiza serikali kupunguza bei ya mafuta.

Hadi kufikia leo haijathibitika kuwepo kwa wimbi au makundi ya watu waliojitokeza kushiriki maandamano. Hakuna kiongozi yeyote aliyejitokeza hadharani na kutoa wito kwa Wananchi kufanya maandamano. Asubuhi ya leo hapajaonekana Rigathi Gachagua na wenzake,  aidha Mwanaharakati Bob Njagi ambaye awali alikiri kuwa mistari wa mbele kushiriki maandamano siku leo hajajitokeza.

# Viongozi wa upinzani na nafasi yao kwenye taarifa hizo

Baadhi ya viongozi wa upinzani nchini Kenya aidha wamesalia kimya kwa kutoa kauli au kujitokeza hadharani. Bila shaka hali hii huenda imechangiwa na hatua za hivi karibuni zilizochukuliwa na serikali  zenye lengo la kupunguza makali ya kupanda kwa bei ya mafuta.

Kwa upande mwingine pia tunaweza kusema kwamba Kuna uwezekano kwamba Viongozi wa Upinzani hawajafikia mwafaka wa pamoja kuhusiana na swala la maandamano au bado wanajipanga. 

Ni vema kusema hapa kwamba Kuna uwezekano Viongozi jawa wakawa na mitazamo tofauti kuhusu maandamano.

Hakuna tamko rasmi la pamoja au la moja kwa moja kutoka kwa viongozi hao kuthibitisha kushiriki au kuongoza maandamano hayo. Ikumbukwe kwamba mara nyingi viongozi hawa wamekuwa wakitoa kauli na matamko ya kuhamasisha ila hawajitokezi kushiriki.

# Hitimisho

Hakuna dalili au uthibitisho kuwepo uwezekano wa kifanyika maandamano leo. Katika kitovu Cha mji wa Nairobi asubuhi hii hali imeonekana kuwa shwari Wananchi wakiendelea shughuli zao za kawaida licha kuonekana Polisi wachache wakishika doria mitaani.

Labda kma hali itabadilika baadaye lakini tathimini ya jumla ni kwamba huenda hakuna maandamano. Ni swala la muda.

Tutaendelea kufuatilia na kutoa taarifa pale ambapo uthibitisho rasmi utapatikana.

Post a Comment

Previous Post Next Post