#NI PASAKA YA HUZUNI NA SIMANZI

#Ajali mbaya yawakosesha Sikukuu ya Pasaka abiria waliokuwa
wakisafiria basi dogo la abiria kwenye Barabara kuu ya Gilgil- Naivasha. 

Siku hizi imekuwa ni jambo la kawaida kusikia kwenye redio, kuona kwenye runinga au mitandaoni taarifa za ajali za mara kwa mara zinazogharimu maisha ya Wakenya. Hali hii imegeuka kuwa janga la kitaifa linalohitaji hatua za haraka na madhubuti  kutoka kwa Serikali, wadau wa usafiri, madereva pamoja na abiria wenyewe.



Taarifa iliyopeperushwa na Vyombo mbalimbali vya Kenya ikiwemo vituo maradufu vya Runinga kama Citizen Tv na NTN Kenya Jumamosi Tar 4 April 2026 zilithibitisha ajali hiyo iliyoua watu 11. Ilikuwa ni siku ya majonzi na simanzi kwa kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao kwenye ajali mbaya iliyotokea kwenye barabara kuu ya Naivasha kuelekea Nakuru, ambapo  walipoteza maisha papo hapo. Ajali hiyo ilihusisha basi dogo la abiria lililogonga lori kubwa aina ya semi-trailer lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara.

Kwa mujibu wa mashuhuda, inaaminika kuwa basi hilo lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi kabla ya kugonga lori hilo, huku baadhi wakidai kuwa hakukuwepo alama za tahadhari za kutosha kuonyesha uwepo wa Lorry hilo kubwa la masafa marefu lililoegeshwa kando ya Barabara hasa Kwa kuzingatia kwamba ilikuwa usiku. 

 Nini Sababu za Kuongezeka kwa Ajali za Barabarani Nchini Kenya Kuongezeka kwa ajali hakutokani na sababu moja pekee, bali ni mkusanyiko wa changamoto kadhaa, zikiwemo:

* Ubovu wa Barabara na Miundombinu katika baadhi ya marneo

*Mwendo kasi kupita kiasi, Madereva wengi hupuuza viwango vya mwendo vilivyowekwa.

*Uzembe wa madereva,  Kutumia simu wakiwa wanaendesha, uchovu au ulevi.

*Ukosefu wa ukaguzi madhubuti wa magari, Magari mengi yasiyofaa huendelea kuruhusiwa barabarani.

*Rushwa miongoni mwa askari wa usalama barabarani, Baadhi ya askari huruhusu magari mabovu kupita kwa kupokea hongo.

*Abiria kutozingatia usalama, Kutofunga mikanda ya usalama licha ya umuhimu wake.

* Ukosefu wa vifaa vya kudhibiti mwendo (speed governors),  Hasa kwenye magari ya usafiri wa umma.

#Uwajibikaji wa Viongozi: Wapi Tumefika?

Waziri wa Uchukuzi wa Kenya, Davis Chirchir, hajaonyesha jitihada za makusudi au mikakati ya kupunguza ajali za Barabarani. Kwa maana nyingine tunaweza kusema na yeye anasikia tu au kuona kwenye runinga kutokana na ukweli kwamba maisha ya wakenya yanazidi kupotea yeye kuonyesha juhudi zake. ,Ndo maana wananchi wengi wanahoji kiwango cha ubunifu na hatua mpya zinazochukuliwa na wizara yake kukabiliana na janga hili.

 Mnamo mwaka 2003/2004, alikuwepo Waziri John Njoroge Michuki ambaye katika kipindi Cha uongozi wake kwenye Wizara ya Uchukuzi alianzisha sheria kali zilizojulikana kama *Michuki Rules*. Sheria hizi zilihakikisha:

* Kila abiria anafunga mkanda wa usalama

* Magari ya umma yanawekewa vifaa vya kudhibiti mwendo

* Nidhamu ya madereva na Makondakita ikiwemo uvaaji wa sare maalum

Swali linalobaki ni je, Kwa nini hatuoni jitihada kama hizi zikirejea au mbinu mpya?


Kwa upande mwingine Waziri wa usalama wa ndani, Kipchumba Murkomen anapaswa kuonyesha uwajibikaji kwa kukomesha rushwa miongoni mwa Askari wa usalama Barabarani. Hatuamini kwamba Waziri hana taarifa au hajui kwamba askari wa usalama Barabarani wanakusanya pesa kutoka kwa kila gari la abiria linalopita kwenye maeneo Yao ya ukaguzi. Kuna taarifa kwamba gari lolote ambalo dereva au kondakta wake hatoi rushwa hufanyiwa mizengwe ya kila aina ikiwa ni pamoja na kubambikiziwa kesi kubwa. Kuna taarifa za kuaminika kwamba huu ni mifumo wa rushwa unaoanzia ngazi za juu na pesa Ile hugawanywa Kwa kuzingatia makusanyo hadi kwa viongozi wa juu wa idara ya Trafiki. 

Askari Hawa ambao huwa na Uswahiba wa kupokea pesa kutoka kwa madereva hao ndo hao hao ambao huwajulisha madereva wenye magari mabovu au ambayo hayakidhi vigezo vya kuhudumu Barabarani kuwakwepa maafisa wa NTSA wanapopanga vituo vya ukaguzi Barabarani. Mara nyingi unaweza kushangaa gari likibadili mkondo wa safari ghafla na kupitia njia nyingine.

Vilevile Hatuamini kwamba viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kama Mkurugenzi Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Mohammed Amin na Inspekta Generali wa Polisi Douglas Kanja, kwamba hawajui au hawana taarifa kuwepo kwa askari wanaochuma pesa barabarani huku wakilipwa mishahara na Serikali. Kwamba katika inteligensia ya nchi hii viongozi hawa hawajui kwamba Kuna rushwa inatembea barabarani.

Je, ni kweli hawajui kuhusu vitendo vya rushwa vinavyoendelea barabarani? Kama wanajua, ni hatua gani wanazochukua kuwawajibisha wahusika?

Mkuu wa idara au kitengo Cha NTSA, Nashon Kondiwa, anapaswa kuchukua hatua madhubuti na kuwekwa mikakati mahsusi ili kupunguza ajali hizi zinazozidi kuangamiza maisha ya wakenya 

#Athari kwa Uchumi na Jamii

Kupotea kwa maisha barabarani si tu maumivu kwa familia bali pia ni pigo kubwa kwa uchumi wa taifa:

* Kupotea kwa nguvu kazi, Watu wenye uwezo wa kuchangia maendeleo ya taifa hupotea ghafla.

*Kuongezeka kwa utegemezi, Familia nyingi hupoteza walezi na kubaki katika hali ngumu ya maisha.

*Kupungua kwa ukuaji wa uchumi, Taifa hupoteza rasilimali watu muhimu.

Inasikitisha zaidi kuona kwamba kwa mujibu wa Takwimu za NTSA, takriban watu 4,311 na 4,458 walipoteza maisha katika miaka ya 2024 na 2025 mtawalia idadi inayoweza kulinganishwa na wapiga kura wa kata au Ward mbili (2) za wapiga kura

# Nini Kifanyike?

Ili kukomesha janga hili, hatua zifuatazo ni muhimu:


1. Utekelezaji uzingatiaji wa sheria za barabarani bila upendeleo

2. Kupambana na rushwa kwa dhati

3. Ukaguzi wa mara kwa mara wa magari

4. Elimu kwa umma kuhusu usalama barabarani

5. Matumizi ya teknolojia kama kamera za mwendo kasi

6. Uwajibikaji wa viongozi wa Umma na taasisi husika

7. Viongozi wabuni sera na mikakati mipya inayoemdana na wakati ili kudhibiti hali.

Post a Comment

Previous Post Next Post