Watu Saba (7) wamefariki Dunia kwa kuuawa kikatili na makundi
ya watu wenye hasira 'Mob justice' baada ya kusingiziwa kuchukua viungo (nyeti hasa za Wanaume) vya wenzao kwa tendo la kuguswa bega. Uvumi huo wa kuwepo kwa watu wanaosadikiwa kuchua nyeti za kiume za wenzao kwa kuwagusa wahusika ulianza kimzaha karibuni wiki moja iliyopita na hadi Kufikia sasa unagharimu maisha ya watu.Hata hivyo Vyombo mbalimbali nchini Tanzania vimechapisha kanusho la Serikali kuhusiana kitokuwepo kwa ukweli wowote huhusiana na taarifa hizo na kufafanua kwamba watu waliodai kunyofolewa au kuchukuliwa viungo vyao walikutwa navyo baada ya kukaguliwa. Akizungumza na waandishi wa habari, msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo, DCP David Miisime amethibitisha kuuawa kwa takriban watu Saba(7) katika matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye baadhi ya mikoa nchini humo na kuwataka Wananchi kujiepusha na uvumi huo.
Si mara ya kwanza kuwepo matukio ya uvumi wa namna moja au nyingine nchini Tanzania unaohusisha Imani POTOFU za kichawi au kishirikina unaosababisha taharuki na mauaji ya watu wasio na hatua.
Miaka 4-5 iliyopita kulitokea uvumi kwamba Kuna watu waliokuwa wakiiba watoto wadogo umri wa mwaka 1 hadi 5 na kuwapeleka kusikojulikana au kiwauza kwa ajili ya makafara. Madhara yake yake waliishia kuuawa hata wazazi husika wa watoto kutokana na kuzushiwa au kutanda kwa taharuki kwa mtu yeyote aliyeonekana na mtoto mdogo, ambapo alivamiwa na kuanza kupigwa kinyama kwa hisia na uzushi bila kujali maelezo yake
Sanjari na hilo serikali ya Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ikipambana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino ) ambayo yamekuwa yakifanyika kwa Imani za kishirikina kutokana na Imani kwamba mauzo ya viungo vya miili Yao ni chanzo Cha utajiri.
